Ijue sheria, haki na wajibu wa domestic workers

Ijue sheria, haki na wajibu wa domestic workers

Ebwana mambo vipi? kama kawaida ikiwa leo ni jumatatu ya mwisho katika mwezi January bwana ambapo siku hii huwa tunaleta zile makala za kazi, ujuzi na maarifa.

Yap leo tutazungumzia moja kwa moja jambo muhimu kabisa ikiwa tunasogezea machoni mwako upate kuzifahamu vyema kabisa zile sheria, haki na wajibu za wafanyakazi wa kazi za ndani.

Fuatilia kwa hatua makala haya ili uweze kujifunza mengi kuhusiana na masuala ya wafanyakazi wa kazi za ndani karibu sana mdau wa mwananchi scoop.

Sasa bwana kwakuanza tumfahamu huyu mfanyakazi wa kazi za ndani ni mtu yoyote anayefanyakazi za nyumbani kama kutunza usafi wa nyumba, mifugo, kufua,kupika au kulea watoto na kupewa ujira/mshahara mwisho wa mwezi au kwa siku kulingana na makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Sheria ya kazi ya Tanzania inawalinda pia wafanyakazi wa kazi za ndani  yaani  (domestic  workers ) kama walivyo wafanyakazi wengine ingawa sheria haijataja specific haki au wajibu wa mwajiri /mwajiriwa wa kazi za ndani.

Sheria ya kazi ya tanzania ( employement and labour relation act  cap 366 r.e 2019 and labour institutions act cap 300 r.e 2019 )  zimeelezea haki na wajibu wa mfanyakazi na mwajiri pahala pa kazi kwa kuonyesha  vifungu vya sheria kulingana na sekta husika au eneo la kazi.

Tanzania ni miongoni mwanachama wa Shirika la kazi duniani (ILO ) hivyo ni lazima kupitisha makubaliano (Convention and Recommendation ) katika kulinda haki za wafanyakazi pahali pakazi.

Kupitia mkataba ( Convention no 189,  Domestic workers convention of 2011)  imeelezea kiundani haki na wajibu wa mfanyakazi wa kazi za ndani, kwanza kabisa kuonyesha  umri sahihi wa mtu kufanya kazi  kwanzia miaka 18  hata chini ya miaka 18 sheria ina mruhusu kufanya kazi zilizo nyepesi pasipo kuathiri afya ya mtu  endapo mwajiri ataenda kinyume na kifungu cha sheria kinavyosema kifungu cha 5(1)&(2) cha sheria ya ajira na uhusiano  kazini (ELRA CAP 366 r,e 2019).

Mfanyakazi wa kaz za ndani anahitajika kupewa mkataba wa kazi unaonesha ukomo wake wa kazi,jina la mwajiri,aina za kazi anazostahiri kufanya ,kiwango cha mshahara imeelezewa zaidi kifungu cha 13 na 14 cha sheria ya ajira na uhusiano kazini (ELRA Cap 366 R,E 2019) iko sambamba na kifungu cha 7 cha mkataba wa kimataifa wa 2011 (domestic workers conv no 189 of 2011).

Licha ya haki za wafanyakazi wa kazi za ndani pia wana wajibu wao katika eneo la kazi kama kuheshimu na kuipenda kazi yake ,kutunza siri za mwajiri,kumuheshimu mwajiri wake na familia kiujumla.

Kiujumla  wafanyakazi wa kazi za ndani na wafanyakazi wengine wanalindwa na sheria kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria za kimataifa.

“Tambua sheria utende haki na kuzingatia wajibu kulingana na nafasi uliyo nayo katika eneo la kazi,kisha fuata sheria”.

Naam kwa leo nimekuandlia hayo ni matuamaini yangu utakua umepata elimu ya kutosha juu sheria, haki na wajibu wa wafanyakazi wa kazi za ndani.

Nakutakia jumatatu njema tukutane tena jumatatu ijayo ya mwezi February kila la kheri mtu wangu wa nguvu kabisaa holaaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post