Ifikapo 2070 dunia itakuwa na watu zaidi ya bilioni tisa

Ifikapo 2070 dunia itakuwa na watu zaidi ya bilioni tisa

Taasisi ya Kimataifa ya Uchambuzi wa Mifumo (IIASA), imeeleza kuwa idadi ya watu duniani inakadiriwa kufikia bilioni 9.4 ifikapo mwaka 2070, licha ya kudaiwa kuwepo kwa ongezeko kubwa zaidi ya makadirio hayo.

Aidha mataifa ambayo yatakuwa na ongezeko na msongamano mkubwa zaidi ya watu ni Pakistan, Indonesia, Marekani, China, na India ambazo zitaongoza kwa ukubwa wa idadi ya watu.

Mwelekeo huu wa idadi ya watu unaonesha kuwa katika miaka hiyo kutakuwa na athari kubwa katika ukuaji wa utamaduni, huduma za kijamii na uchumi.

Hata hiyo kulingana na data kutoka kwa ‘Marekebisho ya Umoja wa Mataifa’ ya 2022 ilieleza kuwa matarajio ya Idadi ya Watu Duniani, inaweza kufikia bilioni 10.4 mwishoni mwa miaka 2080.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post