Ifikapo 2024, Marufuku kutumia Vipes

Ifikapo 2024, Marufuku kutumia Vipes

Serikali nchini #Australia inadaiwa kuwa na mpango wa kupiga marufuku uingizaji  na utumiaji wa #Vipes ifikapo Januari 2024, ikiwa ni sheria mpya za kukomesha ‘vapes’ zinazotumika, kutengenezwa na kusambaza nchini humo.

Vipes zilitengenezwa na kuuzwa kwa watu kama njia ya kuacha kuvuta sigara, lakini Waziri wa afya wa nchini hiyo amesema kuwa imeunda kizazi kipya cha madawa ya kulevya.

Vipes ni sigara za kielektroniki, zinazotumia betri inayounda gesi ya 'erosoli' inayofanana na mvuke wa maji lakini ina nikotini na kemikali nyingine zaidi ya 30, hivyo hutumiwa kama sigara.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post