Ifahamu wine iliyotengenezwa kwa kutumia nyoka

Ifahamu wine iliyotengenezwa kwa kutumia nyoka

Ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni, wakati baadhi ya watu wakitumia mvinyo uliotengenezwa na zabibu kwa ajili ya kujiburudisha, fahamu kuwa wapo wanaotumi mvinyo uliotengenezwa kwa nyoka kumwagilia nyoyo zao.

Mvinyo wa nyoka ni moja ya kinywaji cha tamaduni kinachopatikana China, kinywaji hiki kinaaminika kuwa na uwezo wa kuboresha afya na kuongeza nguvu. Waandaaji hutumia nyoka akiwa hajatolewa sumu kisha kumuingiza ndani ya chupa yenye pombe. Haijalishi akiwa mzima au amekufa

Pombe hiyo ambayo nyoka huwekwa hutofautiana zipo zinazotengenezwa kwa nafaka au matunda na kisha kuhifadhiwa sehemu yenye giza. Mara nyingi hutumia aina za nyoka wenye sumu kama vile Cobra.

Inaelezwa kuwa baada ya nyoka kuwekwa kwenye chupa yenye pombe huachwa kwa muda mrefu ili kuiruhusu sumu na viungo vingine vya nyoka kuchanganyika na pombe kuchachuka. Hatua hii huchukua miezi au miaka kadhaa kulingana na tamaduni, nyoka aliyetumika au mapendeleo ya mtengenezaji.

Inadaiwa mvinyo wa nyoka unatumiwa kama dawa za jadi, hata hivyo inaaminika kuwa na faida za kiafya ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu, kinga, kuboresha mzunguko wa damu, na kutibu magonjwa kadhaa ingawa madai haya hayajathibitishwa kisayansi

Pia watu hupendelea kuutumika kwenye sherehe na matukio maalum kama vile harusi, maadhimisho, au hafla nyingine za kijamii.

Hata hivyo inadaiwa uchachushwaji wa muda mrefu wa mvinyo, hufaya sumu ya nyoka iwe salama kwa matumizi ya binadamu. Hata hivyo watengenezaji watu hutakiwa hazijatayarishwa au kuhifadhiwa kwa usahihi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags