Ifahamu ‘Masaji’ ya nyoka na faida zake

Ifahamu ‘Masaji’ ya nyoka na faida zake

Kwa baadhi ya watu hutumia muda wao kwenda kufanya ‘masaji’ kwa lengo la kuondoa uchovu na kuweka miili yao sawa, na walio wengi wamezoea kufanyiwa ‘masaji’ na binadamu kwa utumia vitu mbalimbali ikiwemo mafuta maalumu ya ‘masaji’ huku muziki wa taratibu ukipigwa.

Kwa baadhi ya mataifa huduma hii ya ‘masaji’ imeboreshwa zaida kwani wateja hawaishii tu kufanyiwa huduma hiyo na binadamu bali hutumia nyoka pia kutoa huduma ya ‘masaji’ na inaelezwa kuwa huduma hiyo ya kutumia nyoka huwa na faida nyingi za kimwili na kisaikolojia.

Mteja ambaye hupatiwa huduma hiyo basi hupakwa mafuta kwenye mwili wake na kisha nyoka  huwekwa juu ya mwili wa binadamu na huanza kutembea katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo usoni.

Huwa na zaidi ya aina 28 ya nyoka wasio na sumu ambao huanza kutumiwa na kisha badae mteja huwekewa nyoka mkubwa aina ya chatu kwa lengo la kukaza misuli na kupunguza maumivu ya mwili kutokana na uzito wa nyoka huyo.

Kwa kawaida masaji hiyo hufanyika ndani ya dakika 20 hadi 40 na wakati mwingine muda huzidi au hupungua kutokana na ombi la mteja.

‘Masaji’ hii ya nyoka huwa na faida kubwa kwa binadamu hasa za kimwili na kisaikolojia na kati ya faida zake inaelezwa kuwa husaidia kuchochea mtiririko wa damu, kuondoa hofu,  kusisimua akili, huimarisha mfumo wa kinga na  husaidia kujiamini hasa kwa wale watu wanaoogopa nyoka, .

Kati ya nchi ambazo zinatoa huduma ya ‘masaji’ ya nyoka ni Egypt, Misri, na Indonesia. Vipi ikija #Bongo unaweza kwenda kuifanya?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post