Ifahamu kazi ya uwazi uliyopo kwenye  mfuniko wa peni

Ifahamu kazi ya uwazi uliyopo kwenye mfuniko wa peni

Wapo baadhi ya watu ambao wakati wa kutumia peni hupendelea iwe  na kifuniko  chake, huku sababu kubwa ya kutaka kiwepo wanadai peni inakuwa nzito hivyo inawapa urahisi wakati wa kuandika.

Pamoja na kutaja sababu hiyo wengi hawafahamu kuwa kifuniko cha peni kimewekewa uwazi juu. kwa mujibu wa tovuti ya India Times, Shirika la Kimataifa la Usalama na Viwango(ISO), limeweka sheria ya peni zote zinazotengenezwa ziwekewe uwazi kwenye vifuniko vyake ili  kusaidia kuokoa maisha ya binadamu.

Kawaida watu wengi hupendelea kutafuta vifuniko vya peni, iwapo kwa  bahati mbaya kifuniko hicho kikimezwa na kukaa kwenye koo kinaweza kusababisha mtu asipumue na mwisho akapoteza maisha.

Hivyo kutokana na uwazi huo  ikiwa kifuniko kitamezwa na kukaa kooni ule uwazi wa juu utasaidia kupitisha hewa japo kwa asilimia ndoto wakati mtu anapatiwa msaada.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na gazeti la The Independent mwaka 2016, nchini Marekani watu 100 huwa wanameza vifuniko vya peni kila mwaka.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post