Ifahamu kampuni inayotoa huduma ya kuwaliza watu na kuwafuta machozi

Ifahamu kampuni inayotoa huduma ya kuwaliza watu na kuwafuta machozi

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, wakati baadhi ya watu wakilalamikia ukosefu wa ajira fahamu kuwa nchini Japan kuna watu wanaendesha maisha yao kwa kufanya kazi ya kuwafanya watu walie na kisha kuwafuta machozi.


Suala la kulia mbele za watu huwa gumu hasa kwa mtu mzima, jambo hili si Tanzania tu inaelezwa kuwa nchini Japan watu wengi ni wagumu kulia na kuonesha hisia zao hadharani, kutokana na hilo mfanyabiashara Hiroki Terai alipata wazo la kuanzisha kampuni yake iliyopo Tokyo Ikemeso Danshi ambayo imeajiri wanaume wenye muonekano mzuri, ambao kikundi chao kinaitwa “Handsome Weeping Boys” kwa lengo la kufanya kazi ya kuwafuta watu machozi taratibu wakiwa wanalia.


Mwaka 2013 Terai alianzisha maonesho ya bure hadharani ya video za kusikitisha za filamu zilizolenga kuwafanya watu walie kwa pamoja na kuonesha hisia zao, kadri miaka inavyozidi kwenda pia huduma yake inazidi kukua kwani kwa sasa ameweza kuajiri vijana wenye umri wa miaka kuanzia 20 wenye muonekano wanaotoa huduma ya kufuta machozi.

Endapo mtu akitaka huduma huwasiliana na kampuni hiyo na kisha kupatiwa muhudumu, na huduma zake hazijaishia majumbani tu bali hadi ofisini huitwa na kuweka filamu za kusikitisha zenye kuwafanya wafanyakazi walie huku wakifutwa machozi.


Lengo la kutoa huduma hiyo Terai anaamini kuwa baada ya kulia na kuruhusu watu kuona udhaifu wako, unaweza kuishi vizuri zaidi na watu nyumbani au kwenye eneo la kazi, inaunda mazingira bora ya kufanya kazi na watu wanaelewana vyema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post