Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga freddy wafikia 200

Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga freddy wafikia 200

Zaidi ya watu 200 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kukumba eneo la kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

Serikali imetangaza hali ya maafa katika wilaya 10 za kusini ambazo zimeathiriwa zaidi na kimbunga ikiwemo kituo cha kibiashara cha Malawi, Blantyre, ambacho kimerikodiwa kuwa na vifo vingi Zaidi.

Mashirika ya misaada yanaonya kwamba uharibifu huo utaongeza mlipuko wa kipindupindu nchini Malawi huku wafanyakazi wa uokoaji wamezidiwa, na wanatumia majembe kujaribu kuwatafuta manusura waliofukiwa na udongo.

Shirika la misaada la kimatibabu la Madaktari Wasio na Mipaka lilisema kuwa zaidi ya watoto 40 walitangazwa kufariki walipofika hospitalini.

Aidha Viongozi wametoa wito kwa familia zilizoachwa kuchukua maiti kwa ajili ya mazishi kwani chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo kinakosa nafasi.

Shirika la serikali la kusaidia maafa limesema zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post