Huyu ndiye rafiki wa kweli kwa Rambo

Huyu ndiye rafiki wa kweli kwa Rambo


Wakati baadhi ya watu wakichagua marafiki wa kuwanao katika maisha kwa ajili ya kuwasaidia lakini hii ilikuwa tofauti kwa mwigizaji mkongwe wa Marekani Sylvester Stallone ‘Rambo’ ambaye kwa upande wake aliamua kujenga urafiki na mbwa kwa zaidi ya miaka 10.

Wakati akiwa anafanya kazi kwenye moja ya mgahawa uliyopo New York City, Rambo alimuokota mbwa mdogo aina ya ‘Bull Mastiff’ na kumpatia jina la mchezaji mpira wa miguu la Dick Butkus.

Kupitia mahojiano yake aliyowahi kuyafanya miaka ya nyuma Rambo aliweka wazi kuwa Butkus alikuwa rafiki yake bora kuwahi kutoka kwani alikuwa akiwa naye kwenye nyakati ngumu na za furaha na hata zile alizokuwa akiandika skripti ya filamu ya Rocky mwaka 1976.

Urafiki wa wawili hao uliendelea mpaka pale Rambo alipokata tamaa ya kuishi ambapo alichukua jukumu la kumuuza mbwa huyo kwa Dola 40 nje ya duka la 7-Eleven.

Baada ya filamu ya Rocky kuuza na kupata maokoto ya kutosha, alifanikiwa kumrudisha tena kwa kumnunua dola 15,000 huku akiweka wazi kuwa mbwa huyo alistahili kununuliwa kwa kiasi hicho cha fedha.

Butkus alionekana katika Rocky na Rocky II kabla ya kufariki mwaka 1981, hata hivyo Rambo bado anasema Butkus alikuwa kama mtoto wake wa kwanza ambapo amemweka screensaver (picha ya mbele kwenye simu) hadi leo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags