Huyu Ndio Justin Bieber Wa Lulu

Huyu Ndio Justin Bieber Wa Lulu

Tangu kuanza kwake muziki msanii wa Canada, Justin Bieber alikuwa akiwachanganya mabinti wengi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mwonekano wake, huku akiwamaliza zaidi kwa wimbo wake ‘Baby’.

Moja ya wasichana waliokuwa wakivutiwa naye ni mwigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alikuwa akionesha mapenzi yake waziwazi kwa msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii.



Wakati mitandao ya kijamii hasa X (zamani twitter) ikianza kuiteka dunia. Mwaka 2013-14 mwigizaji huyo aliwahi kuandika machapisho ambayo yalijidhihirisha kuwa alimpenda Bieber kimapenzi.

“Hivi wewe Justin Bieber mbona unajishaua sana?, ni kwamba huoni tweet zangu au ndiyo mapozi, siyo kesi lakini mimi nakupenda hivyo hivyo. Halafu nakusoma mitandaoni unavyofanya mambo yako ya ajabu wivu ninao na roho inauma pia.

"Justin Bieber Tanzania nzima wananiona chizi kwa jinsi ninavyokupenda, Tanzania unapajua lakini? hope ulitusikia juzi kati Rais wako alivyokuja. Hata kama umenichunia sikuachi ng’o ntakomaa na wewe kama Shilole anavyokomaa na Jiji la Dar” aliwahi kuandika Lulu kupitia Twitter yake

Aidha Lulu aliendeleza machapisho hayo licha ya kujua kuwa msanii huyo tayari alishaingia katika mahusiano na mwanamuziki na bilionea Selena Gomezi huku akisisitiza zaidi kuwa yeye ndio anampenda kwa dhati.

Kwa takribani wiki sasa mwonekano wa Bieber umekuwa ukizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kama mzee wa miaka 40 licha ya kuwa na miaka 30 kwa sasa.

Mwonekano huo umewafanya mashabiki wake kujawa na maswali huku wengi wakionesha kumuonea huruma. Ikumbukwe 2023 msanii huyo alitangaza kusumbuliwa na ugonjwa wa ‘Ramsey Hunt Syndrone’ ambao unapelekea mwonekano wake haswa uso kuoneakana umezeeka kutokana na maumivu na miwasho anayoipata usoni.

Mbali na hayo msanii huyo amewahi kufanya vizuri na ngoma zake kama vile Baby, Sorry, Yummy, Never Say Never, Lonely, One Time na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags