Huyu hapa mwanaume aliyeruka ukuta kuingia chumba cha Malkia

Huyu hapa mwanaume aliyeruka ukuta kuingia chumba cha Malkia

Ni kawaida binadamu kujaribu vitu hata vile ambavyo wengine hudhani haviwezekani , hasa wakitaka jambo lao lifanikiwe. Duniani kote inafahamika kuwa sehemu anayoishi Rais, Malkia au Mfalme huwa na ulinzi mkali ambao si rahisi kuingia bila sababu za msingi.

Wakati watu wengine wakiwa na hofu ya kusogea katika lango la ikulu bila sababu ya msingi kutokana na ulinzi mkali, fahamu kuwa yupo mwanaume mmoja aliyewahi kuingia kwenye Kasri la kifalme (Buckingham Palace), yalipokuwa makazi hayati Malkia wa Uingereza Elizabeth II, na kuzama hadi chumbani alikolala Malkia.

Mwanaume huyo anafahamika kama Michael Fagan bila wasiwasi Julai 9, 1982 majira ya saa moja asubuhi alipada ukuta mrefu wa Kasri wenye mita 4.3 na kuzama mpaka ndani bila ya walinzi kumuona.

Walinzi wakiwa na mitutu yao mkononi, Michael aliweza kupenya na kutafuta njia ya kuingia ndani kwa kupanda juu ya paa na baadaye alifanikiwa kuingia ndani kwa kupitia dirishani, uzuri wa mjengo ule ulimchanganya na kujikuta akizunguka na kushangaa kila mahali.

Katika harakati zake za kushangaa alifika hadi katika ofisi ya Malkia, akaamua kujipumzisha kwenye kiti cha enzi cha Malkia katika kutupa macho huku na kule Michael aliona chupa ya mvinyo mweupe aunywao, ndipo akajimiminia na kuanza kumwagilia moyo taratibu.

Utalii wake kwenye jumba hilo ukaendelea katika vyumba vingie, ndipo akakiona chumba alicholala Malkia, Michael alizama hadi kwenye chumba hicho na kuanza kumshangaa Malkia kwa ukaribu zaidi, akakaa

pembeni ya kitanda alicholala Malkia huku kiganja chake kikiwa na damu aliyoumia wakati wa harakati za kuingia ndani.

Muda si mrefu Malkia aliweza kushituka na kumkuta jamaa kakaa pembeni akimshangaa ndipo alianza kupiga kelele huku  akitaka msaada kwa walinzi. Hata hivyo inaelezwa mlinzi cha chumba cha Malkia siku hiyo aliwahi kutoka zamu kabla ya mwingine kufika.

Ndipo walinzi walifika na kumuweka kumkamata huku kila mmoja akiwa anajiuliza ameweza vipi kuingia kwenye mjengo huo, Michael alishitakiwa kwa kosa la wizi wa kunywa mvinyo wa malkia na kutakiwa kufanyiwa uchunguzi wa akili huku akiwa chini ya ulinzi kwenye hospitali ya watu wenye matatizo ya akili ndani ya miezi mitatu na baadaye kuachiwa.

Jambo la kuingia ikulu bila ruhusa halikuhesabika kama kosa kwa sababu kipindi hicho hakukua na sheria iliyoeleza kuwa ni kosa la jinai kufanya hivyo. Katika moja ya mahojiani Michael alieleza lengo lake lilikuwa ni kukaa na Malkia na kumueleza matatizo yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post