Sanaa ya ucheshi kwa baadhi ya watu imekuwa ikiwaminisha kuwa hata nje ya majukwaa wachekeshaji kila wanachokifanya wanakuwa wanafanya masihara.
Ikiwa leo ni Alhamis siku ambayo watu hukumbuka baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea siku au miaka ya nyuma, leo tukumbuke tukio la mchekeshaji Thomas Frederick Cooper aliyefariki akiwa jukwaani anachekesha na baada ya kudondoka mashabiki waliendele kucheka na kushangilia wakijua ni mbinu ya uchekeshaji.
Mchekeshaji huyo na mwanamazingaombwe, Thomas Cooper, mara nyigi alitumia jukwaa kuonesha ucheshi wake na kufanya matukio ya ajabu kwa watu waliokuwa wakimtazama.
Kama ilivyo kawaida ya wachekeshaji kuchukuliwa kila wanachofanya ni utani ndicho kilichomkuta mchekeshaji huyo Aprili 15, 1984.
Inaelezwa kuwa mwishoni mwa mwaka 1970 Thomas alikuwa akivuta sigara na kunywa pombe kupita kiasi, jambo ambalo liliathiri kazi yake na afya yake.
Na Tarehe 15 Aprili 1984, alifariki akiwa na umri wa miaka 63 baada ya kupata mshtuko wa moyo akiwa jukwaani anafanya ucheshi mbele ya zaidi ya watu milioni 1, huku tukio hilo likiwa linaonekana live kwenye kwenye kipindi cha London Weekend Live.
Kipindi hicho kilikuwa kikirusha matukio moja kwa moja kutoka ukumbi wa Her Majesty's, Westminster, London, ambako ndiko, mchekeshaji huyo alikuwepo.
Baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo Thomas alidondoka chini na kuanza kutapatapa lakini hakuna msaada wowote aliopata kwani mashabiki wake waliamini kuwa ilikuwa ni mbinu moja wapo ya kuchekesha.
Waliendelea kuangua kucheko, hadi alipokata roho bila wao kujua.Baada ya muda kupita bila ya kunyanyuka huku vicheko vikiendelea ndipo Jimmy Tarbuck, Alasdair MacMillan (mkurugenzi wa utayarishaji wa kipindi hicho kwenye Tv), na wafanyakazi waliyokuwa nyuma ya pazia waligundua tukio hilo, kuwa si sehemu ya kichekesho walisogea, huku vicheko vya watazamaji vikaanza kupungua.
Lakini Thomas hakuweza kunyanyuka na kugundulika kuwa tayari alikuwa amepoyeza maisha.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply