Huu ndio mitindo tofauti wa mavazi ya rais Bukele

Huu ndio mitindo tofauti wa mavazi ya rais Bukele

Hellow!!it’s furahidayy, haya sasa kwa mara nyingine tena tunakutana this weekend huku mambo mengine ya kiendelea na sisi team Scoop hatuja poa tunaendelea kukupasha yaliojiri na yanayojiri ulimwenguni.

Leo katika fashion tunakuletea kitu cha tofauti kidogo kama ulivyozoea mara nyingi tunafahamu kwamba viongozi wa nchi au serikali duniani hawanaga muda wa mambo ya mitindo kwa sababu mavazi yao yanaeleweka.

Kama ulikuwa unafikiri cheo kinaweza kumuweka kando mtu na mitindo mbalimbali ya mavazi, utakuwa bado hujasikia kuhusu Rais Nabiy Bukele.

Buleke ni rais wa nchi ya El Salvador ambayo inapatika Amerika ya kati ambayo hadi mwaka huu inakadiriwa kuwa na watu milioni 6.5.

Alizaliwa Julai 24, 1981 katika mji mkuu wa nchi hiyo San Salvador katika familia ya kitajiri yenye asili ya Palestina.

Alipata elimu yake ya sheria kutoka Central American University, baada ya chuo alianza kufanya biashara na kufungua makampuni na baadae alijiingiza katika siasa na kuchaguliwa kuwa Meya katika jiji la Salvador na baadae kujitosa kuwania nafasi ya urais.

Anatajwa kama moja ya raisi mdogo duniani ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 43 na amekuwa moja kati ya mwanasiasa ambaye amejizoelea umaarufu ulimwenguni kutokana na aina yake ya mavazi.

Imezoeleka viongozi wa kisiasa wanapokuwa katika maeneo mbalimbali haswa katika mikutano ya hadhara huonekana wakiwa wamevalia mavazi rasmi, lakini hii imekuwa tofauti kwa Buleke.

Anapotokea katika mikutano, matukio na hafla za ndani na nje ya nchi mara nyingi huonekana akiwa amevalia jeans na tshirt au shati huku akiwa ametupia miwani pamoja na kugeuza kofia yake wakati akiivaa.

Pale anapoamua kuvalia suti mara nyingi hapendelei kuvaa tai kama anavyoonekana katika picha zake nyingi zilizopo mitandaoni.

Uvaaji wake huo umefanya kupata umaarufu mkubwa duniani na kupendwa zaidi haswa na kundi la vijana na kupelekea  baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kumpachika jina la rais bishoo.

Amekuwa ni mmoja kati ya wanasiasa mwenye umri mdogo  ambao wamekuwa na wafuasi wengi katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa upande wa Instagram hadi sasa amefikia wafuasi milioni 4.8 huku Twitter akiwa na milioni 5.1.

Jina hilo lilishika umaarufu zaidi baada ya kujipiga selfie baada ya kumaliza kutoa hotuba kwenye mkutano wa umoja wa mataifa (UN).

Hata hivyo alipohojiwa na baadhi ya vyombo vya habari alidai  kwamba hiyo picha ikienda Instagram itapeleka ujumbe  kulizo hizo hotuba wanazo toa.

Tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa pamoja na uvaaji wa rais huyo lakini amekuwa moja kati ya mwanasiasa mfano wa kuigwa kwa vijana kutokana na mapambano yake dhidi ya vitendo vya rushwa kuhakikisha usalama wa raia wake dhidi ya makundi ya kijambazi. Rais bishoo anaishi kikawaida na ana swagga kama vijana wa sasa.

Hata hivyo mtaalamu wa masuala ya mitindo ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema mavazi anayovaa rais huyo hayana tatizo kama hayakiuki mila na desturi za sehemu anayotoka.

Alisema pengine aina ya mavazi ambayo ameonekana kupendelea kuyavaa yamechagizwa na umri wake mdogo.

"Yuko katika rika la vijana pengine ndiyo sababu anapendelea kuvaa nguo hizo cha msingi zinatakiwa tu ziwe hazikiuki mila na desturi za nchi hiyo"amesema.

Hata hivyo mwanamitindo chipukizi Jackline Maneno anasema kuwa ni muhimu mtu kuvaa kulingana na tukio au shughuli anayoenda.

"Kama tukioni rasmi basi inashauriwa kuvalia nguo rasmi ili kurndana na shughuli iliyopo"aliongeza.

Haya mwenetu usiwaze sana kuhusu mitindo ya mavazi sasa hivi kwa wale vijana wenye ndoto ya kuwa na vyeo  muhimu usikiuke mila na desturi ya sehemu unayotoka lakini kwa hapa Tanzania je akatokea kiongozi moja akawa na swaga za Rais Buleke unafikiria itakuaje embu njoo tulijadiri katika mitandao ya kijamii @Mwananchiscoop kwa kudondosha komenti yako mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags