HOW TO GET MORE INSTAGRAM FOLLOWERS

HOW TO GET MORE INSTAGRAM FOLLOWERS

Habari kijana mwenzangu!Je unatamani kupata followers wengi kwenye account yako ya instagram na  hutambui namna ya kupata followers wengi?  Soma kwa makini dondoo hii ili uweze kutambua namna gani unaweza kufanikiwa kwenye hilo.

Hii ni fursa kwako wewe kijana ambaye  unandoto za kuanzisha biashara ya  mitandaoni ,ili uweze kuendesha biashara  yako kupitia njia ya mitandao basi hakiksha unakuwa na wafuasi wengi kwenye akaunti yako ili uweze kupata wateja wengi,Tumia njia hizi hapa kufikia malengo yako.

 Fuata mshawishi ( follow influencer)

Hii ni njia ya kwanza na nzuri sana kuitumia itakayokuwezesha kupata wafuasi wengi kwa muda mfupi, anza kufollow watu wengi wenye tiki za blue ambao mara nyingi huwa ni watu maarufu kadri unavyowafollow ndiyo followers wanavyoongezeka kwenye akaunti yako. 

 Tangaza akaunti yako kwenye mitandao mingine

Njia nyengine ni kutangaza akaunti yako kwenye mitandao mingine kama facebook itakusaidia kujulisha wateja wako kuwa umefungua akaunti nyengine ni njia ya kuongeza wafuasi wengi zaidi.

 Tumia hashtags(#hashtags)

Matumizi ya hashtags pia yatakusaidia kuongeza followers kwenye akaunti yako, ni vyema kutumia hashtags pale unapokua unapost  picha au video kwenye ukurasa wako wa instagram.

Pendelea kukomenti na kulike kwenye picha za watu mbalimbali.

Hii ni njia ambayo itakusaidia  hakikisha unalike na kukometi kwenye picha za watu ambao wako kwenye nchi yako ili uweze kuongeza wafuasi jitahidi angalau picha 50 za kwanza kila siku utaona matunda yake.

 Hakikisha unazingatia muda wa kuposti vitu vyako

Kuanzia saa saba mchana ni muda mzuri wa kuposti kwani wakati huu ndiyo muda wa chakula cha mchana au wengine wanakua wameshapata mlo na hutumia muda huu kuangalia simu zao kabla ya kurejea kwenye majukumu yao.

Pendelea kuposti zaidi siku za wikiendi

Mara nyingi siku kama jumapili watu wengi wanakuwa mitandaoni ili kuangalia taarifa mbalimbali hivyo ni vyema kutumia wakati huu kuongeza wafuasi kwenye akaunti yako, kwa kuposti picha na video mbalimbali.

  Hakikisha bio (biography) yako imekamilika.

Hapa unatakiwa kuandika  taarifa zako zote muhimu kuhusiana na akaunti yako,inajihusisha na nini ili iwe rahisi hata mtu akiwa anatazama profile yako basi anapata taarifa zote zinazohusiana na kitu ambacho unakifanya.

Hivyo basi kwa kuzingatia hayo unaweza kufanikisha azma yako, nakutakia siku njema.

 

 






Comments 2


  • Awesome Image
    Mellomarsh49

    🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥#Nomaaa Nikubayaaaaaa

  • Awesome Image
    Mellomarsh49

    🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥#Nomaaa Nikubayaaaaaa

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags