Hivi ndiyo viatu vyenye gharama zaidi duniani

Hivi ndiyo viatu vyenye gharama zaidi duniani

Tumezoea kuona bei za kawaida wakati wa kwenda kununua viatu, huku baadhi ya watu wakijiwekea ukomo wa kiatu anachotaka kununua kisizidi bei Fulani. Sasa leo Mwananchi Scoop tumekusogezea viatu ambavyo vinatajwa kuwa na gharama zaidi duniani.

Kwa kujibu wa tovuti ya Forbes imetoa listi ya viatu 5 vyenye gharama zaidi kwa mwaka 2024
1. Moonstar Shoes vinathamani ya dola 19.9 milioni ikiwa ni sawa na Sh 51.3 bilioni


Viatu hivi ambavyo vinashika namba moja kuwa vya gharama, kwa mara ya kwanza vilioneshwa mwaka 2019 katika maonesho ya Wiki ya Mitindo ya MIDE (Made in Italy, Designed in Emirates) yaliyofanyikia kwenye boti, Dubai.

Viatu hivyo vinatajwa kuwa vimetengenezwa na dhahabu imara na kupambwa na vipande vya almasi 30.

2.Jada Dubai and Passion Jewellers Passion Diamond shoes vinathamani ya dola 17 milioni sawa na Sh 43.8 bilioni


Kwa mara ya kwanza vilioneshwa katika hoteli ya Burj Al Arab, hoteli pekee ya nyota 7 duniani, vimetengenezwa kwa dhahabu halisi na kupambwa kwa almasi 240.

3.Debbie Wingham heels vinathamani ya dola 15.1 milioni sawa na Sh 38.9 bilioni


Heels hizo zilioneshwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 na kuuzwa katika familia ya kitajiri kutoka Dubai ambayo haikutajwa jina, walinunua viatu hivyo kwa ajili ya zawadi ya siku ya kuzaliwa.

Viatu hivyo vinagharama hiyo kutokana na kutengenezwa kwa dhahabu na zaidi ya vipande 1,000 vya almasi.

4.Shoes thrown at President George W. Bush vinagharama ya dola 10 milioni sawa na Sh 25.8 bilioni


5.Harry Winston Ruby slippers vyenye gharama ya dola 3 milioni sawa na Sh 7.7 bilioni


viatu hivi vilitengenezwa mwaka 1989 huku mtengenezaji akitumia miezi miwili kuweka rubi 4,600 pamoja na almasi 50, mara ya kwanza vilivaliwa na Judy Garland.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post