Hivi ndivyo Diamond alivyompa mchongo Dr Almas

Hivi ndivyo Diamond alivyompa mchongo Dr Almas

Na Masoud Kofii

Bongo Fleva na Bongo Movie ni tasnia zinazofanya kazi kwa kushirikiana nchini, kutokana na muingiliano wa baadhi ya mahitaji ya kikazi mfano namna ambavyo waigizazji wanatumiwa kwenye video mbalimbali za wasanii wakubwa nchini hususa kwa kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imechukua nafasi kwa ukubwa.

Lakini pia wasanii wa muziki kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakionekana kwenye tasnia ya filamu nchini kwa kuigiza na wakati mwingine nyimbo kutumika kama sound track kwenye filamu mbalimbali.
Hivi karibuni iliachiwa video ya wimbo ‘Ololufemi’ wa kwake Jux akiwa kamshirikisha Diamond Platnumz. Wimbo ambao umefanya vizuri kuanzia audio ambayo ilianza kutoka na kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya wakali hao kumpata mwongozaji makini nchini Fole X kazi ya kusimamia video hiyo ndipo alipata wazo la kumtumia mwigizaji Dr.Almas katika kichupa hicho.

Dr.Almas mwenye umri wa miaka 61 katika video hiyo ya Ololufemi akapewa jukumu kucheza kama baba wa Jux na Diamond. Akizungumza na Mwananchi Scoop mwigizaji huyo amesema alipata bahati ya kuonekana kwenye wimbo huo kwa sababu ya ukubwa wake kwenye tasnia

" Nimecheza kama baba Jux na Diamond na kama King wa Kinageria alafu nikawa na machief ambao nimewapa jukumu la kuwatafutia warembo watoto wangu lakini watoto wangu wakawa na machaguo yao ya wapenzi wengine ambao walikuwa wanataka kuoa, mfalme nikashindwa, story ilitaka kuonesha nguvu ya mapenzi," amesema Dr. Almas

Hata hivyo licha ya Tanzania kuwa na waigizaji wengi wenye umri wake Almas amesema wasanii hao walimchagua yeye kutokana na ubora wake
"Unajua unapomuongelea Dr.Almas unazungumzia "The Baddest Dady in Town" na mtu mwenye sanaa yake na Diamond ni mtu anayependa vitu vizuri walitafuta mtu bora wakaniona mimi alivyopelekwa picha tu akakubali bila kupinga tukapanda mezani na kuandika deal tukafanya kazi kama unavyoona video tumeuwa kinoma yaani" amesema Dr.Almas

Kutokana na kuonekana kwenye video ya wakali hao, Dr Almas anasema imemfungulia milango mingi kwani simu za michongo zimeanza kuita
"Kuna simu kadhaa zimeita kuna series itakwenda Netflix tunatakiwa kwenda kuichezea Monduli itakuwa ya kimila na asili nitacheza kama King kama kwenye Ololufemi nahisi jamaa aliniona kwenye Ololufemi kwa hiyo akapenda nitacheza kama muhusika mkuu ," amesema Dr.Almas
Mbali na uigizaji Dr.Almas ni mtamu pia kwenye mitindo ya mavazi.

"Mimi niliamua kutengeza dunia yangu mwenyewe kwenye maswala haya ya fasheni huwa najichungulia najicho la nguo kwa sasa nina designer wangu anatokea Arusha kwenye kuvaa kila mmoja ana namna yake labda swagga zangu zinawakamata Wabongo.

“Mimi ni mnyamwezi tangu mdogo na haya ndio maisha yangu sijadandia maisha, kuzeeka ni amri ya Mungu na kuzeeka ni baraka na kumbuka kwamba tutazeeka wote kuna kundi kubwa linapukutikia njiani kwahiyo zeeka ila shine utakavyoweza usikubali kuchakaa,"amesema

Dr. Almasi anaongezea kuwa licha ya kuwa na muonekano huo yeye ni baba wa watoto watatu Jackson, Berinda, na Brenda na watoto wake wote amewalea katika mazingira ya heshima huku akitimiza wajibu wake kama baba

"Sijui watu wanachukuliaje, unyamwezi sio uhuni lakini mimi ni baba wa familia nina watoto watatu na watoto wangu ni kama washikaji zangu hamna kitu wananificha kwasababu nimeshuka kwenye maisha yao kama mshauri wao, "amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags