HABARI njema kwa wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani, namna gani unatakiwa kujiandaa ili kuhakikisha unafanya vizuri na kufaulu kwa kiwango cha juu katika mitihani yako?
Bila shaka mwanafunzi yoyote Yule duniani ili apimwe kile ambacho amejifunza lazima apatiwe jaribio au maana nyengine mtihani kwa ajili ya kupima uwezo wake juu ya somo husika.
Leo nitakujuza mbinu chache ambazo unaweza kuzitumia na kufanya vizuri katika kipindi ambacho unajiandaa kufanya mitihani yako itakayokupa kibali cha kutimiza ndoto yako.
Leo nakuletea dondoo tano muhimu zitakazokusaidia wakati unafanya maandalizi ya kuelekea kwenye Mitihani hiyo.
>Jipe muda wa kutosha wa kujisomea
Hakikisha unaandaa ratiba yako ya masomo kwa kipindi hiki cha mwisho kulingana na mitihani itakavyoanza kuazia somo la kwanza hadi la mwisho, usiache chochote kwa dakika ya mwisho.
>Jitahidi kupitia mitihani iliyopita
Njia bora zaidi ya kujianda kwa mitihani ni kufanya mazoezi na toleo la zamani la mitihani iliyopita, jaribio la zamani litakusaidia kuona muundo na uundaji wa maswali na itakuwa vizuri kwako kujua nini cha kutarajia kufanya kwako mazoezi itakusaidia kupima muda unaohitaji kwa mtihani halisi
>pendelea kusoma kwa vikundi na marafiki
Hii ndiyo njia pekee ambayo inaweza kukusadia katika kuelekea kwenye mitihani yako ya mwisho, Vikundi vya masomo vinaweza kukusaidia kupata majibu unayohitaji na kumaliza kazi haraka zingatia kikundi kinazingatia somo husika na hawakuvurugi.
> Panga siku ya mitihani yako
Hapa sasa zingatia sheria na mahitaji yote ya mitihani,hakikisha unafika kwenye eneo lako la kufanyia mitihani mapema ili kuondoa wasiwasi nahofu au uwoga utakao sababisha kujichanganya ukiwa katika chumba cha mitihani.
>Tenga muda wa kupumzika
Mapumziko ya kawaida yanahitajika ili ubongo urejeshe umakini wake, Sio mbinu bora kusoma masaa mengi kwa sababu uhifadhi wa maarifa kwa muda mrefu hauwezekani. Sehemu muhimu zaidi ya kusoma ni kukuza utaratibu unaofaa mtindo wako wa kusoma.
Mwanafunzi mwenzangu ili uwezekufanikiwa zaidi zingatia hili, wakati wa kusoma unashauriwa kunywa maji kwa wingi ni muhimu na inaimarisha afya yako kiujumla.
Nakutakia maandalizi mazuri na mafanikio makubwa katika kipindi cha usoni wako katika kila la kheri watahiniwa wenzangu.
Leave a Reply