Mnamo mwaka wa 2010, mkono wa profesa mmoja nchini India ulikatwa na watu wenye hasira kali baada ya kushutumiwa kwa kuutusi Uislamu katika mtihani alioutunga.
Mwezi uliopita, serikali ililipiga marufuku kundi lenye utata la Kiislamu la Popular Front of India (PFI), ambalo wanachama wake walikuwa wamefanya shambulio hilo.
Onyo:
Makala hii inamaelezo ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kuhuzunika.
TJ Joseph anakumbuka vyema shambulio la miaka 12 iliyopita. Ilikuwa asubuhi ya Julai yenye mvua. Prof Joseph, ambaye wakati huo alikuwa mwalimu wa lugha ya Kimalayalam mwenye umri wa miaka 52 katika chuo cha eneo hilo, alikuwa akiendesha gari nyumbani akiwa na mama yake na dada yake baada ya Misa ya Jumapili huko Muvattupuzha, mji wa kupendeza katika jimbo la kusini la Kerala kwenye kingo za mto unaoitwa Kerala .
Takriban mita 100 kutoka kwa nyumba yake kwenye njia yenye majani mengi, inayoteleza, gari dogo la Suzuki likiendsa kwa kasi na kusimama kuizua hatchback ya TJ. Wanaume sita walishuka na mmoja wao alikimbia hadi kwenye gari la Prof Joseph, Alikuwa amebeba shoka.
Yule mtu alipoukaribia mlango wa dereva na kujaribu kuufungua kwa nguvu, mtu mwingine aliyeshika jambia akaja upande wa nyuma. Wengine watatu walifika upande wa abiria alipokuwa amekaa dada yake.
Dirisha la upande wa dereva likavunjwa vipande vipande kwa pigo la shoka, Prof Joseph aligundua kuwa alikuwa amevamiwa.
Madaktari walitumia masaa 16 kushona na kuunga mkono wa Prof Joseph
Awalimburuta na kumtoa nje ya gari na kumshambulia sana, ikiwemo kumkata mkono wake wa kushoto na kuutupa. "Nilijiuliza, yote ni kweli na yanatokea," Prof Joseph alisimulia.
Baada ya shambulio hilo, wale watu walitokomea na Majirani walimchukua Prof Joseph na kumpeleka hospitali. Mkono wake uliokuwa umekatwa ulipatikana kwenye bustani ya jirani ukiwa "kama jani lililokaushwa", uliwekwa kwenye begi na kukimbizwa hospitalini kando.
Alikuwa katika hali mbaya, akitukaa hospitalini kwa siku 35 kutibu majeraha.
"Uhalifu wangu ulikuwa ni kuuliza swali kwenye mtihani wa wanafunzi ambalo baadhi ya watu walidhani liliukashifu Uislamu. Hilo liliinua maisha yangu," Prof Joseph aliniambia. Awali kulikuwa na majaribio matatu ya kumvamia Prof TJ nyumbani kwake
Miezi minne kabla ya shambulio hilo, Prof Joseph aliamshwa na simu mapema ilikuwa Machi 26. Alikuwa mkuu wa Chuo cha Newman, kinachoendeshwa na kanisa la Katoliki la Roma, na ambapo alikuwa katika mwaka wa pili wa kazi yake ya tatu katika taaluma ya ualimu iliyodumu kwa miaka 25.
Mkuu wa chuo alimwamnbia kwamba mapolisi walikuwa wamejaa katika eneo la chuo, na ingekuwa bora kama angekaa mbali. "Mambo yanaweza kuharibika ikiwa utakuja," mkuu wa shule alionya.
"Kwa nini? Sijafanya chochote kibaya," Prof Joseph aliuliza. Mkuu wa shule akamwambia "wanasema kwamba Mtume ametukanwa na mabango yamebandikwa kwenye ukuta wa chuo".
Swali la kuudhi lilikuwa zoezi la majaribio ya mtihani ambapo Prof Joseph aliweka mazungumzo ya kufikirika kati ya "Mungu na mwendawazimu" - kutoka kwenye kitabu cha kilichoandikwa na mtengenezaji wa filamu PT Kunju Muhammed.
Alimpa"mwendawazimu" huyo jina la Muhammed, anasema, ambnalo ni jina pili la muongoza filamu PT Kunju. "Muhammed ni jina la kawaida miongoni mwa Waislamu. Haikuniingia akilini kwamba mtu yeyote angeelewa vibaya hilo kuwa ni Mtume Muhammad," Prof Joseph alisema.
Wanafunzi thelathini na wawili wakiwemo Waislamu wanne walikuwa wamefanya mtihani huo. Hakuna hata mmoja wao aliyepinga jambo hilo; na ni mwanafunzi mmoja tu wa kike "aliyeonyesha kusitasita
Watu 31 walikama kwa kumshambulia TJ, huku 10 wakihukumiwa miaka 8 kila mmoja jela
Maandamano makubwa yaliibuka, ghasia na Polisi waliokuwepo chuoni walikuwa na lengo la kuzuia ghasia za waandamanaji waliokwenda na mabango ya kulalamika alichokiandika TJ katika mtihani.
Ilimlazimu atoroke ana familia yake, akihama mji mmoja kwenda mwingine, lakini siku ya 6 baadaye ilibidi kujisalimisha Polisi ambapo walikwend akupekuwa nyumbani kwake na kuchukua vitu kadhaa ikiwemo hati yake ya kusaifiria.
Baada ya wiki moja ya kukaa jela, alitoka kwa dhamana na kwenda kuishi kwa wakwe zake, akihofia kutoka nje kwa usalama wake, walikuwa wnaataka kumuua.
Watu sita walishakuja mara kadhaa kumuulizia wakijifanya wanafunzi wake. Ilimpa hofu na kuitaarifu Polisi waliomuhaidi kufanya doria mara kwa mara katika eno analoishi.
Alikuwa na mama yeke mzee, licha ya kushauriwa na majirani aondoke, hakutaka kumuacha nyuma.
Picha hii ni siku ya 35 aliporuhusiwa kutoka Hospitali baada ya kushambuliwa
Takriban mwezi mmoja baada ya Prof Joseph kurejea kutoka hospitali , chuo chake kilimfukuza kazi. Kulikuwa na dhoruba ya maandamano huko Kerala: walimu walichangisha pesa kwa ajili ya matibabu yake; barua za msaada na kumfariji kwa kuwekwa ndani zilimiminika; watu mashuhuri wa kifasihi na kitamaduni walishutumu kufukuzwa kazi; na waandamanaji wawili walifanya mgomo wa kula nje ya chuo chake.
"Ni kundi la watu wasiojali ambao wangeweza kupuuza hali hizi zenye kudhuru na kumfukuza kazini wakati ana mke na watoto wawili wa kuwatunza," gazeti la ndani liliandika katika tahariri.
Kwa Profesa maisha yalikuwa magumu na kupururuka kwa haraka. Hana kazi.
Mkewe Salomi Joseph ( kulia), alipatwa msongo wa mawazo na kujiua
Huko nyumbani, mke wake anayeitwa Salomi, aliyekuwa na umri wa miaka 48, aliingia katika msongo wa mawazo. "Alisema anataka kufa," Prof Joseph alisema.
Familia hiyo iliondoa dawa za kuulia wadudu zilizowekwa nyumbani, ikaficha visu vyote, ikafunga dawa zake, ambazo Prof Joseph pekee ndiye angeweza kuzipata. Yote haya haikusaidia. Alasiri moja mnamo , baada ya kula chakula cha mchana, Salomi alijiua. Kifo chake kilizua ghadhabu kubwa, huku chuo hicho kikilaumiwa kwa masaibu ya familia.
Lakini siku tatu baada ya kifo chake, hatimaye Prof Joseph alirejeshwa kazini na chuo hicho. Alikuwa na siku tatu kabla ya kwenda kustaafu.
Dayosisi ya Kikatoliki ya eneo hilo ilishikilia msimamo wake.
Ilisema katika barua ya wachungaji iliyosomwa katika makutaniko kwamba swali la Prof Joseph "lilichanganya kufuru na matusi ya kidini" na "kusababisha huzuni kwa wanafunzi wa jamii fulani". Dayosisi hiyo, barua hiyo ilisema, "imemuonea huruma na kumrejesha katika utumishi" kwa "mazingatio ya kibinadamu" na sio kwa sababu kulikuwa na shinikizo la umma walioandamana.
Kurejeshwa kwakwe kazini kwa siku hizo tatu kulimaanisha alikuwa na haki ya kupokea mishahara yake yote na stahiki zake za miaka 4 iliyopita tangu wamfukuze.
Prof Joseph akiwa na dada yake na mkwewe nyumbani kwao huko Kerala
Maisha yametulia sasa familia ya Joseph. Prof Joseph anasema "amezaliwa upya" kama mwandishi. Akiandika kurasa 700 kwa mkono wake wa kushoto, alikamilisha kumbukumbu zake - "A Thousand Cuts", - ambazo zilitolewa mwaka jana na kupata sifa kubwa na tangu wakati huo ameuza zaidi ya nakala 30,000.
Pia amechapisha muendelezo wa "slimmer, mostly satirical" . Sasa anapanga kutoa kitabu chake cha hadithi fupi.
Chanzo BBC
Leave a Reply