Hilda Baci kufungua chuo cha mapishi

Hilda Baci kufungua chuo cha mapishi

Mpishi maarufu ambaye alijuliakana zaidi baada ya kuvunja rekodi ya kupika kwa muda mrefu Hilda Baci anatarajia kufungua chuo cha mapishi ambapo darasa la kwanza linatarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

Chuo hicho ambacho kimepewa jinala ‘ Hilda Baci Academiy’ kitafundisha mapishi zaidi ya 160, huku akiweka wazi kuwa dhumuni la kufungu chuo hicho ni kutaka kuwasaidia wanawake ambao wanaamini kuwa kuna mafanikio katika kupika.

Hilda alipata umaarufu mwaka wa 2023 baada ya kuvunja rekodi na kuingia katika kitabu cha rekodi ya dunia cha ‘Guinness World Record’ (GWR) kwa kupika masaa 100 bila kupumzika lakini rekodi hiyo ilivunjwa na Alan Fisher ambaye alipika siku nane sawa na saa 199.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post