Hiki ndiyo kimemfanya Barnaba kuhamia kwenye filamu

Hiki ndiyo kimemfanya Barnaba kuhamia kwenye filamu

Mwanamuziki Barnaba Classic ambaye kwa sasa ni mwigizaji wa filamu ya Mawio inayorushwa Azam Tv amesema kuwa kabla ya kuanza muziki alikuwa mwigizaji

“Nilikuwa mwigizaji kabla ya kuimba muziki, nilitoa kwanza filamu ndio nikaja kuwa mwimbaji, kwahiyo hakuna sababu yoyote zaidi ni kufanya kazi yangu inayoendelea tuu kwa sababu sikuwahi kutaka kufanya uigizaji na ndio maana nikajikita kwenye muziki,” amesema Barnaba Classic

Aidha mwanamuziki huyo ameweka wazi kuwa sababu nyingine ya kugeukia kwenye filamu ni dau nono ambalo aliwekewa.

“Lakini cha pili kilichonifanya niingie katika soko la filamu dau limekuja kubwa kwa hiyo sikuona sababu ya kulikwepa kwa sababu uhusika waliyonipatia niliona kabisa naweza kuucheza,” alisisitiza Barnaba ambaye anatumia jina la Bob Ed au Alawi Beach Boy katika filamu ya Mawio.

Wapo baadhi ya mashabiki wanaamini kuwa Tamthiliya ya Mawio ndio filamu ya kwanza kwa Barnaba Classic lakini amefunguka kuwa aliwahi kufanya filamu nyingi lakini nyingine hazikuwahi kutoka.

“Nimewahi kuigiza filamu nyingi lakini nyingine hazikuwahi kutoka moja ambayo imewahi kutoka na ninakumbukumbu nayo ni filamu inayoitwa ‘Yatima wa Roho’” amesema Barnaba Classic.

Aidha mwanamuziki huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani kwa sasa gari limewaka ambapo ameahidi kuendeleza kipaji chake cha uigizaji kwa kutoa filamu mbalimbali.

Barnaba Classic ameendelea kutamba na kujulikana zaidi baada ya kuachia albumu yake ya ‘Love Sounds Different’ ambayo amefanya kolabo na wasanii wenzie akiwemo Diamond, Nandy, Jux, Alikiba na wengineo huku ngoma kama Hadithi, Sijiwezi, Marry Me, Tamu, Sayuni zikifanya vizuri kupitia mitandao mbalimbali.

Kwa sasa Barnaba anatamba na ngoma ya ‘Nibusu Remix’ aliyomshirikisha Mbosso na Yammi yenye zaidi ya watazamaji milioni 1.1 katika mtandao wa YouTube ikiwa na wiki mbili tu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post