Ayaaaah!! Huku ndiko walikotokea bwana wakina Madonga mtu kazi, bila kumsahau shujaa wake Shabani Kaoneka. Hivi umewahi kujiuliza mchezo wa ndondi, ngumi au masumbwi ulitokea wapi na ilikuwaje jamii ikaukubali mchezo huu na kuaminika kama michezo mingine?
Maana mchezo wa ngumi bwana unahitaji uzoefu kidogo na wewe mwenyewe kama uliwahi kujaribu jaribu hata kuingia ulingoni na jirani laasivyo bhanaa unaweza kuangukia pua.
Hahahahaha, natania lakini ni matani ambayo ukifikiria yanashabihiana na ukweli wa mchezo huu leo bhana nakuletea historia fupi ya mchezo huu tangu ulipoanza kutambulishwa rasmi kwenye jamii hususani hapa kwetu Tanzania.
Twende tuufahamu sasa mchezo huu ni mchezo wa aina gani na unabeba watu wangapi wakati wakucheza, fuatilia hapa utajua tu.
Mchezo wa ngumi ni aina ya michezo ya mapigano ambapo mabondia wawili wanapigana kwa kutumia ngumi pekee yaani mkono ndiyo unaotumika zaidi hapo kwa kushirikiana na viungo vingine japo sio kivileee mzee baba, sijui unanielewa?
Hahahah!! Usije ukaingia ulingoni baada ya kuona mambo si mambo ukataka kumpiga mtu kichwaaa mzee baba utatolewa ulingoni hahaha, nakukumbusha tu ndugu yangu usijekujisahau ukazua balaa zaidi.
Huu ni mchezo ambao unachezwa lakini kwa kufuata kanuni na taratibu za mchezo huo kwani hapo wote wawili mnatakiwa kuvaa gloves nene kwa shabaha ya kupunguza hasara za kiafya.
Haya sasa, mchezo huu kama nilivyokueleza kuwa unahusisha mafahali wawili lakini hawakai zizi moja hahaha utasema leo mwandishi mbona anadadavua hivi naye anacheza ngumi nini? Kumbeee wapiii ushabiki tu mwenzangu.
Hahahaha hapana hata mimi navutiwa sana na mchezo huu, sijui wewe msomaji wangu! owkey tuangalie sasa mashindano yake yanasimamiwa na nani wakati wadau wakiwa ulingoni pale.
Unaambiwa bwana mashindano ya mchezo huu husimamiwa na refa, kwa kawaida mbele ya watazamaji na kutekelezwa kwenye ulingo maalumu kabisaa asikwambie mtu kuhusu pambano hili bhanaa.
Lakini bwana mashindano yake yamegawanyika kwa vipindi vinavyodumu dakika 1-3 ambapo shabaha ya mchezo wa mashindano ni kumshinda mpinzani katika uwanja wa mchezo bila kumuumiza mno yaani kumpa jeraha za kudumu.
Nikukumbushe tu kuwa azimio la ushindi limo mikononi mwa refa yaani namaanisha (mwamuzi) anayesimamia mashindano na kuhakikisha kwamba kanuni zinafuatwa.
Michezo hii ya mapigano bwana mara nyingi inatumia faini za sanaa ya mapigano.
Vilevile kanuni siku zote zinahakikisha yakwamba washindani wana uwezo wa kulingana, hivyo wanapangwa mara nyingi kwa ngazi mbalimbali kulingana na uzito wao.
Watu waliwahi kupigana unaambiwa zama hizoo kwa kutumia ngumi lakini kwakufuata kanuni fulani tangu millennia nyingi kwa mujibu wa historia.
Aiseee hivyo ndivyo mambo yalivyokua ila sasa jinsi mchezo huu ulivyoenea kote duniani kwa sasa, tambua kuwa ulianza huko nchini Uingereza katika karne ya 19.
Mifano ya michezo ya ngumi ni kama vile mwereka, judo au karate pia michezo mingi ya mashindano yanayotumia mikono, miguu au hata mwili kwa ujumla.
Hivi unafahamu kibongo bongo mchezo huu ulianza mwaka gani?
Ndondi bwana zilianza miaka ya 1964, kipindi hicho ambapo George Anautoglo aliwapa wananchi ukumbi kwa ajili kwa ajili ya vijana kukutana na kufanya mazoezi kipindi hicho wakati anawakabidhi vifaa vya mazoezi akasahau vifaa vya ngumi.
Hussein Mapepe alikuja na glove na jezi, watoto wengi wakazipenda ndipo George Anautoglo akaamua kununua vifaa vya ngumi na watoto wengi waliupenda mchezo huo hadi leo unachezwa.
Mwenyekiti wa ngumi kipindi hicho alikuwa Desai Jaluo na katibu wake Nizar Walji huku wachezaji walikuwa Titus Simba, Salim Seif Mkamba, John Zembetakis, Kasim Saidi na Jack Raymond.
Aiseee hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa nimekupa tu idea kidogo na kukufumbua macho kuhusu mchezo huu kama unataarifa nyingine zaidi unaweza kutuambia kupitia ukurasa wetu wa Instagram @MwananchiScoop. Its Friday make some noise weuweeee!!!!!!!!!!
Leave a Reply