Hii hapa maana ya jina la albumu ya Wizkid

Hii hapa maana ya jina la albumu ya Wizkid

Mwanamuziki wa Nigeria Wizkid ameandika historia nyingine katika tasnia ya muziki wa Afrobeats kwa kuachia albamu yake ya sita leo Novemba 22, 2024 iitwayo ‘Morayo’.

Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard imeeleza kuwa Wizkid ameamua kuiita album hiyo Morayo neno la Kiyoruba lenye maana ya ‘Ninaona Furaha’ kama heshima kwa marehemu mama yake Juliana Morayo aliyefariki Agosti 2023.

Albumu hiyo ina nyimbo 16 inayojumuisha vibao vilivyotangulia kutolewa kama Piece of My Heart, Bad Girl, Bad for You, Après Minuit na nyinginezo.

Wimbo “Piece of My Heart” uliopo kwenye albumu hiyo umefikia nafasi ya nne kwenye chati za U.S. Afrobeats Songs na nafasi ya saba kwenye World Digital Song Sales, huku Asake na Wizkid wakipata uteuzi katika tuzo za Grammy 2025 kwa wimbo bora wa muziki wa Kiafrika kupitia “MMS”.

Katika uzinduzi rasmi wa albamu hiyo uliofanyika Lagos, Wizkid alitangaza ziara ya kimataifa inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao akiahidi kuwafikia mashabiki wake duniani kote,
“Muziki wangu ni hadithi za Afrika zinazovuka mipaka kupitia Morayo nataka ulimwengu ujue tunaweza kupenda, kusherehekea, na kusimama imara licha ya changamoto,” alisema.

Morayo inakuja miaka mitatu baada ya albamu yake ya mwisho ya More Love, Less Ego, ambayo ilifikia nafasi ya pili kwenye chati za World Albums na nafasi ya 59 kwenye Billboard 200 huku nyingine ambazo aliwahi kuzitoa ni pamoja na Made in Lagos na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags