Haya ndiyo maradhi yaliyoondoa uhai wa mwigizaji Fredy

Haya ndiyo maradhi yaliyoondoa uhai wa mwigizaji Fredy

Kufuatia kifo cha mwigizaji Fredy Kiluswa kilichotokea jana Novemba 16,2024 katika hospitali ya rufaa Mloganzila, mwongozaji msaidizi wa tamthilia ya 'Mizani ya Mapenzi' Alex Mgeta 'Ngosha' amesema mpendwa wao alikuwa akisumbuliwa na moyo.

Ngosha ambaye ni mwongozaji msaidizi wa tamthilia hiyo aliyokuwa akiigiza marehemu
Fredy ameiambia Mwananchi marehemu aligundulika kuwa na ugonjwa huo miezi miwili iliyopita.

"Alikuwa na shida ya moyo, alikuwa anaumwa muda kama wa miezi miwili nyuma alitibiwa akajisikia nafuu akarudi uraiani, akaanza kutumia dawa kama kawaida baadaye ikafikia hiyo hali ambayo siyo nzuri ndiyo ikamletea matokeo haya lakini awali alikuwa afanyiwe oparesheni wataalamu wakaona wampe kwanza dawa akaendelea vizuri kabisa baadaye gafla hali ikabadilika.

"Mara ya mwisho presha yake ilikuwa juu sana kwa hiyo wakati ipo juu wataalamu lazima waisubiri ishuke ili waendelee kutoa matibabu, ikasubiriwa ishuke wakafanya wanaloweza kufanya lakini haikuleta matokeo ambayo tuliyatarajia,"amesema Ngosha

Hata hivyo, hadi sasa bado hakuna taarifa rasmi ya sehemu ambayo msiba utafanyikia mpaka pale familia itakapokaa kikao.

"Msiba kuna mawili jana tulikuwa tumetoka hospitali tukawa hapa kwa mama yake mdogo lakini kwa mzee wake ni Mbagala kwa hiyo msiba unaweza ukahamia Mbagala au ukabakia hapa kikao ndiyo kitatoa maamuzi ubaki hapa au uende huko," amesema Ngosha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags