Ikiwa tunaelekea kuumaliza mwaka 2023, wapo baadhi ya wasanii ambao wanatamani mwaka huu uishe ili wajaribu tena mwakani lakini wapo waliobahatika kuandika historia kwenye vitabu vyao kutokana na mafanikio waliyopata mwaka huu.
Licha ya kuwepo waliozingua na waliofanikiwa lakini unaweza sema mwaka 2023 umekuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, na kuwapatia mafanikio baadhi ya wasanii kwa kujizolea madili ya ubalozi na kujibebea tuzo kadha wa kadha ndani na nje ya nchi.
Tuzo hizo ambazo zimeendelea kuimarisha heshima kwenye kazi wanazofanya na kuwaongezea hali ya kujituma zaidi ili kuleta ladha ya muziki mzuri kwa mashabiki wao. Kwa kulitambua hilo jarida hili la Mwananchi Scoop tumekuletea tatu bora ya wasanii alioongoza kupokea tuzo kwa mwaka 2023.
Diamondplatnumz
kwa mwaka 2023 Diamond amekamilisha jumla ya tuzo tano ambazo tatu zikiwa zinatoka nje ya Tanzania na moja ndani ya nchi. Tuzo ya kwanza aliyopata Simba la Masimba Dangote ni tuzo ya Best African Act Award kutoka MTV European Music Awards, ambayo inakuwa tuzo ya tatu sasa kwa Mondi kupokea kutoka MTV/EMA, jambo linalofanya awe msanii wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya tuzo za MTV/EMA.
Ambapo mbili aliwahi kupokea mwaka 2015 kwa usiku mmoja kama Best African Act na Best Worldwide Act (African/India).
Mbali na hiyo ya MTV mkali huyu kwa mwaka huu ameweza kuibuka kidedea na tuzo ya Best Artist East Africa, kutoka Trace award zilizofanyikia Kigali Rwanda octoba 21. Tuzo ya Best Male View’s Choice Digital kutoka Tanzania Music Awards zilizotolewa jijini Dar es salaam April 29.
Mkali hajaishia hapo akasepa tena na tuzo ya Collaboration Of The Year kutoka Tanzania Music Awards kupitia wimbo uitwao “Nitongoze” aliofanya na Rayvanny. Mwisho ni tuzo ya Best Female East Africa , kutoka Afrimma Awards zilizotolewa Dallas, texas septemba 17. Kwa ujumla inakamilisha tuzo tano za Simba kwa mwaka 2023.
Zuchu
Wakumuita ‘Honeyyy’ naye si kinyonge Zuchu anaongoza gurudumu kwa wasanii wa kike kwa kujizolea tuzo nyingi mwaka 2023 ambazo zote ni kutoka Tanzania Music Awards na kuwa na jumla ya tuzo tano ambazo ni Best Bongo Fleva Song Of The Year kupitia wimbo wa Kwikwi, Best Female Artist , Best Female Bongo Fleva Of The Year, Best Music Video Of The Year kupitia wimbo wa Mwambieni, na Best Female Viewer’s Choice Digital.
Harmonize
Bila ya kuwa na konakona nyingi Konde Boy 2023 pia amekuwa msanii aliyeongoza kwa kusepa na tuzo nyingi kwa mwaka huu na kupelekea jina lake kuendelea kujizolea umaarufu kwenye mataifa mbalimbali.
Mwaka huu mkali huyu wa Bongo fleva ameweza kujishindia tuzo tatu nje ya nchi na moja ndani ya nchi jumla amepata tuzo nne kwa mwaka 2023. Upande wa tuzo za African Entertainment Awards, USA (AEAUSA), zilizofanyika Marekani, NewJersey November 11, alijizolea tuzo ya Best Music Video kupitia wimbo wa ‘single again’, tuzo ya Best Artist of the Year na Afro Bongoking of East Africa.
Haikuishia hapo pia alijibebea tuzo ya Best Male Musician of the Year, kutoka Tanzania Music Awards zilizofanyika jijini Dar es salaam Aprili 29.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply