Harmonize awatolea povu wanaodai anaendeshwa na mapenzi

Harmonize awatolea povu wanaodai anaendeshwa na mapenzi

Msanii wa Bongo Fleva Harmonize amewatolea uvivu wanaodai kuwa anamawazo ya mapenzi, amesema katika ma-ex wake hakuna wa kumfanya alewe.

Konde amefunguka hayo kupitia Instastory yake na kueleza kuwa ana kila kitu katika maisha yake mafanikio, ndugu, mtoto, nyumba, magari na hata pesa hivyo siyo mbaya kwake kunywa pombe maana kwa upande wake ni burudani.

Aidha Harmonize ameweka wazi kuwa ameeleza hayo kwa sababu ameanza kuona comment za watu wakidai kuwa anakunywa sana pombe kwa sababu ya mawazo ya mapenzi, ametengua kauli hiyo na kusema kuwa ma-ex wake wote ni washikaji wake na ni suala la maamuzi tuu arudi kwa ex gani maana hakuna wa kumfanya alewe.

Ikumbukwe Harmonize aliwahi kumvisha pete muigizaji maarufu nchini Kajala na mahusiano yao kuishia kati baada ya wawili hao kugombana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags