Harmonize atangaza ujio wa tamasha lake

Harmonize atangaza ujio wa tamasha lake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize ametangaza ujio wa tamasha lake ambali litafanyika Februari 14 mwakani.

Tamsha hilo ambalo limepewa jina la Afro East Carnival litajumuisha wasanii mbalimbali kutoka nchini Afrika Mashariki.

Harmonize ametoa taarifa hizo kupitia Insta Story yake kwa kuandika “Afro East Carnival 14/02/2022 Dar es Salaam jiji la Amos Makalla let’s go meet all the biggest East Afrika Artists in One Stadium,”

Basi tuambie msomaji wetu hivi ungependa kukutana na msanii gani kutoka Afrika Mashariki kwenye tamasha hilo, dondosha comment yako kwenye ukurasa wetu hapo ambao ni @mwananchiscoop.

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags