Harmonize atamani kufanya kazi na Meek Mill

Harmonize atamani kufanya kazi na Meek Mill

Mwanamuziki wa #BongoFleva, #Harmonize ameamua kuzama DM ya ‘rapa’ kutoka Marekani #Meekmill akiomba kufanya naye kazi ya muziki.

Kupitia #Instastori ya Harmonize ame-share Screen short ya maongezi yake na ‘rapa’ huyo ikionesha shauku kubwa ya kutaka kufanya kazi na Meek ambaye alionesha kutomfahamu Konde kwa kumuuliza anafanya sanaa gani Afrika.

Endapo wawili hao watafanikiwa kufanya kazi kwa pamoja basi itakuwa siyo ngoma ya kwanza kwa Harmonize kufanya ‘kolabo’ na wasanii wa nje kwani amewahi kufanya kazi na ‘rapa’ kutoka Marekani #BobbyShmurda kupitia wimbo wake wa  ‘I Made its’ uliyotoka miezi minne iliyopita.

Mbali na hilo naye ‘rapa’ RickRoss aliwahi kumtaja Harmonize kuwa ndiye msanii anayemkubali kutoka Afrika.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags