Harmonize apiga marufuku wimbo wa Yanga Bingwa kupigwa popote

Harmonize apiga marufuku wimbo wa Yanga Bingwa kupigwa popote

Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize amepiga marufuku wimbo wake wa ‘Yanga Bingwa’ kupigwa na kuchezwa sehemu yoyote mpaka pale atakapo toa taarifa.

Harmonize ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram saa chache baada ya mchezo wa Yanga na Tabora United kumalizika jana Novemba 8, kwa Yanga kuchezea magoli 3-1.

“Warning sitaki wimbo wangu wa ‘Yanga Bingwa’ upigwe sehemu yoyote sio kumbi za starehe wala sehemu yoyote yenye mkusanyiko mpaka nitakapo wajulisha asanteni sana natarajia ushirikiano ndugu DJS ngoma za kupiga ni nyingi mno pigeni hii mpya ya @officialnandy” ameandika Konde Boy

Lakini pia Harmonize ameonesha kuchukizwa na kitendo cha msanii Tundaman kutumia wimbo huo wa ‘Yanga Bingwa’ kwa kuweka mistari inayowabeza mshabiki wa Yanga kwa matokeo hayo mabaya.

“Tunda Man ametumia biti ya Yanga anthem na melod YANGA HII UNAIFUNGAJE bila kunishirikisha wala ruhusa yoyote nikimfikisha Mahakamani ntakuwa namuonea?? Sina shida na hela ila inani disturb makolo wanautumia huo wimbo kwenye matokeo haya mapya mabaya kwetu nakuheshimu Tunda futa huo wimbo please” amemalizia Konde

Harmonize aliachia wimbo wa Yanga Bingwa miezi mtatu iliopita kama sehemu ya kukaribisha wachezaji wapya na kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania 2024/2025






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags