Harakati za MJ mfalme wa pop anayetamba hadi leo

Harakati za MJ mfalme wa pop anayetamba hadi leo

Ikiwa leo ni Septemba 5 2024, Alhamisi ya 36 tangu kuanza kwa mwaka huku zikiwa zimebaki siku 117 kuumaliza mwaka.

Upande wa TBT tunamuangazia mwanamuziki Michael Jackson, maarufu kama "Mfalme wa Pop," aliyezaliwa Agosti 29, 1958, huko Gary, Indiana, Marekani.

Mkali huyo wa Pop alianza muziki akiwa na umri wa miaka tisa kama mwanachama wa kundi la Jackson 5 lililohusisha ndugu, akashiriki kwenye vibao maarufu kama vile "ABC" na "I Want You Back."

Lakini, ilipofika miaka ya 1980 ilimuweka MJ kwenye ramani ya kimataifa kama msanii wa solo. Huku Albamu yake ya nne, "Off the Wall" (1979), ikiwa ni mwanzo wa mafanikio yake na albamu ya tano, "Thriller" (1982) baada ya kutoka ikafanya vizuri zaidi.

Hata hivyo "Thriller" haikuwa tu albamu yenye mauzo makubwa zaidi kwa wakati huo, pia ilivunja rekodi za nyingi za muziki, ikiwa na nyimbo kama "Billie Jean," "Beat It," na "Thriller" yenyewe.

Baada ya hapo umaarufu wa MJ uliendelea kuvuka mipaka kutokana na ubunifu wake hasa kwenye video zake.

Ikumbukwe Video za "Thriller" na "Billie Jean" zilionesha ubunifu wa hali ya juu na hadi sasa bado zinawavutia baadhi ya wato. Mfano kwenye "Thriller," video yake ilikuwa na ngoma maarufu ya zombies ambayo ilivutia mashabiki na kuweka alama kwenye historia ya muziki.

Lakini mbali na uimbaji wake mfalme huyo pia alijijengea utambulisho kutokana na mavazi aliyokuwa akipendelea kuvaa kama yale makoti ya suti na kofia za mduara pamoja glove. Utambulisho wake mwingine ulitokana na mtindo wa kucheza uitwayo "moonwalk," ambao ulipata umaarufu baada ya kuufanya kwenye onesho la 'Motown 25: Yesterday, Today, Forever' mwaka 1983.

Hata hivyo, ifahamike kuwa staili hiyo ya Moonwalker huchezwa kwa kumuonesha msanii kama anatembea kwa kurudi nyuma. Licha ya kuwa mtindo huo ulipewa umaarufu na MJ lakini ulikuwa unachezwa tangu miaka ya 1970, na wanamuziki kama vile James Brown na Cab Calloway.

Mbali na hayo licha MJ kupata mafanikio mengi alikumbana na changamoto, kama vile mashtaka ya unyanyasaji wa kingono, kashfa na magonjwa lakini bado kazi zake zimeendelea kuishi, amefanikiwa kupata zaidi ya tuzo 700. MJ alifariki dunia Julai 25, 2009.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags