Halep afungiwa miaka minne, Kosa utumiaji wa madawa

Halep afungiwa miaka minne, Kosa utumiaji wa madawa

Mchezaji wa Tennis na bingwa wa zamani wa Wimbledon, Simona Halep amefungiwa kutokujihusisha  na mchezo huo kwa muda wa miaka minne kutokana na matumizi ya dawa za kuongeza uwezo katika mchezo huo.

Halep alisimamishwa tangu Oktoba mwaka jana baada ya majibu ya vipimo kuonyesha kuwa alitumia dawa kinyume na sheria.

Hivi karibuni Wakala wa Kimataifa wa Uadilifu na Nidhamu katika mchezo wa Tennis umethibitisha kuwa nyota huyo amefungiwa hadi Oktoba 6, 2026.

Ingawa mchezaji huyo amekana makosa hayo na kusema kuwa hakubaliani na kufungiwa kwake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags