Hakika Reuben  "Sifagilii ustar"

Hakika Reuben "Sifagilii ustar"

 “Sijawahi kutamani kuwa maarufu (star), wala sifurahishwi sana na maisha ya kuwa mtu maarufu katika jamii kwani sio maisha bora kwangu nayakumbuka maisha yangu ya kawaida kabla sijawa maarufu”.

 Hiyo ni kauli ya Hakika Ruben, mchekeshaji aliyejizolea umaarufu hivi karibuni  kupitia mtandao wake wa kijamii wa “Tiktok” ambapo hadi sasa amefikisha wafuasi zaidi ya elfu arobaini na tatu.

Hakika ameeleza wazi licha yakuwa na umaarufu mkubwa wa kuburudisha  anayatamani  maisha yake ya hapo awali kabla hajawa maarufu.

“Nayatamani sana maisha yangu ya  awali mimi ni mkimya sana sijazoea maisha ya kujichanganya na watu tofauti tofauti kitendo cha kuwa maarufu kinanipa wakati mgumu sana".

"Sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuwa mchekeshaji ila hii staili yangu ya kuishi watu wameipenda ndo imenifikisha hapa nilipo kwa sasa"anasema.

 Vile vile Hakika ruben ni mchekeshaji ambaye mara nyingi hupenda kuwasilisha ujumbe kwa hadhira akionyesha maisha yake halisi  jambo ambalo limeweza kuwavutia  watu  wengi.

 “Nina miezi kadhaa sasa tangu nianze kutambulika kikubwa nashukuru jamii imenipokea vizuri jambo   ambalo sijategemea kwani nilikua nafanya vichekesho  kama sehemu ya maisha yangu”.

Aidha aliongeza kuwa kitu kilichobadilika baada ya kutambulika katika jamii kwa sasa ameweza kupanua wigo wa mawasiliano.

"Mimi nilikuwa naishi maisha yangu mazuri tu kikubwa nimepata faida ya kuwa na watu wengi wanaonifahamu kwa sasa, kama kuhusu suala la maisha mazuri nilikuwa nayo  tangu  hapo awali."

Huku akiongeza  kuwa watu wanaomzunguka kwa sasa ni tofauti na hapo awali alivyokuwa  japo imekua changamoto kwake kuyakabili mazingira mapya ya kikazi.

"Mwanzoni  nilikua nagombana na watu wa kawaida kama majirani zangu lakni sasa hivi najikuta napambana na waigizaji wenzangu nimepanua  wigo wa marafiki na Maadui pia".

Hakika ameweka wazi kuwa anavipaji vingi licha ya kuwa mchekeshaji yeye ni Muigizaji wa sinema za mfululizo (series movie) na  muimbaji wa nyimbo za injili (gospel).

Vile vile ameongeza kuwa ukiachana na uwezo aliokuwa nao  yeye kama kijana anajishughulisha  na shughuli nyengine wanazozifanya vijana wa kitanzania.

"Kama kijana hajawa dereva bodaboda au bajaji basi atakuwa

 anauza duka aidha languo,  kibanda cha uwakala au masuala ya IT hizo ndo kazi zetu hata mimi niko ndani ya shughuli hizo".

Hata hivyo hakika amefafanua suala la yeye kuwa anashirikiana na kampuni ya asasi akidai kuwa yeye anafanyakazi kwenye asasi hiyo.            

Wasifu wake 

Hakika Rubeni ni mzaliwa wa mkoa wa Iringa kabila lake ni Muhehe  na ameloweya nchini kenya kikuyu kwa wakamba ambapo alifanikiwa kusoma elimu yake ya awali hadi sekondari.

Aidha Hakika amezaliwa mnamo mwaka 1993 na anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kila ifakapo tarehe 25 mwezi 4 ya kila mwaka.

Pia Hakika ni  mtoto wa kwanza Kati ya watoto watatu katika familia  yao akiwa na wadogo zake wawili akiwemo  Twilu Reuben na Moab Reuben.

Changamoto

Akizungumzia kuhusu changamoto ambayo anaipata tangu alipoanza kutambulika kwa jamii Hakika anaeleza kuwa mvutano baina  ya watu ndiyo tatizo kubwa kwake (tension).

"kiukweli mimi ni mkimya sana sasa kitendo cha kujichanganya na  watu kinanipa  ugumu sana kwani hapo awali sikuzoea kuishi maisha ya  namna hiyo."

Ndoto yake

Ndoto yake  anatamani sana  kukutana na mchekeshaji  mkubwa hapa bongo ambaye anatambulika kwa jina la  Idris Sultan kwani anamkubali sana kutokana na namna anavyofanya kazi zake za uchekeshaji. 

"Kiukweli  mastaa ni wengi hapa bongo lakini natamani sana kukutana  nae kwa sababu namna anavyofanya kazi zake naona kabisa anashabihiana na mimi kwani mimi napenda mtu anichekeshe kama ninavyofanya kazi zangu lakini sio mtu adhamirie kunichekesha."anasema

Akizungumzia aina mbalimbali ya  uchekeshaji ambao unafanywa  na baadhi ya wasanii wa kiume  kupenda kuchekesha kwa staili ya kuvaa uhusika wa kike yeye anaeleza kuwa bado hajawahi kufikiria  kufanya aina hiyo ya uchekeshaji.

"Kila msanii na staili yake ya kuchekesha wengine ili wanoge zaidi inawalazimu kuvaa uhusika wa kike ila binafsi yangu bado sijafikiria kufanya hivyo kwa sababu hakuna kitu kitakachoashiria nifanye aina hiyo lakini ikitokea ntaangalia na uzito wa jambo lenyewe kama litanilazimu sana ila mimi sipendelei aina hii"

Maisha na Mahusiano

Hakika ameeleza wazi kuwa hajawahi kuoa ila alifanikiwa kuishi na mwanamke na kubahatika kupata watoto watatu na wawili wakiwa bahati mbaya walifariki.

Hakika aliongezea kuwa kwa sasa nimebakiwa na mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka saba(7)ambaye tayari ameanza kupata elimu yake ya Msingi.

Vile vile amebainisha kuwa kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yoyote yule na endapo ataingia basi mashabiki na watu wake wakaribu watagundua hilo.

"Kiukweli sijawahi kudeti na wanawake watatu kwa wakati mmoja na nikisema niingie kwenye mahusiano basi wote mtajua kwani nikiwa kwenye mahusiano hua siwi na mambo mengi hata kuposti hamtaona mara kwa mara".

Aidha alielezea kuwa changamoto ambayo anaipitia na anashindwa kuingia kwenye mahusiano ni kutokana na watu ambao anakuanao huwa wanamzungumzia kuwa yeye ni mtu wa kulalamika sana.  

" wanawake wengi wanasema mimi nina malalamiko yani nina wivu sana na ukweli mimi nikimganda mtu na mng'ang'ania haswa" anasema.

 

Usichokijua kuhusu hakika

Hakika amewahi kubeba uhusika wa kaka kwa aliyekuwa mzazi mwenzake kwenye msiba wa mtoto wao baada ya kutambulishwa yeye kama kaka na mwanamke ambaye alizaa nae.

“Sitaweza kusahau jambo hili mzazi mwenzangu alinitambulisha mimi kama kaka yake baada ya kuolewa na mwanaume mwengine wakati wa msiba wa mtoto wetu”.

“Niliumia sana lakini nilitumia ubinaadamu huwezi kuleta fujo msbini lakini baada ya tukio hilo sikuruhusu tena mtoto wangu aliyebaki kuendelea kukaa kwa mama yake niliamua kumchukua mwanangu”.

Ili kupata habari zinahusu wasanii wakongwe na chipukizi hapa bongo, endelea kufuatilia jarida la Mwananchi Scoop ili ufahamu mengi zaidi.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags