Hadatha:  Kuwa Msanii mkubwa ni ndoto inayo ishi moyoni mwangu

Hadatha: Kuwa Msanii mkubwa ni ndoto inayo ishi moyoni mwangu

Name; Hadatha Mylose

Birthday; January, 14

Kazi; Musician 

Oooooyeeeeeah! It’s another friday mwendo ni ule ule hatupoi wala hatuboi, basi bwana leo kwenye kile kipengele chetu pendwa cha mjue zaidi yani hapa tunakusogezea wasanii chipukizi na wale masuper star wa bongo na nje ya bongo, ambapo utaweza kujua kuhusu mambo yao kem kem.

Leo bwana tunakusogezea mwanadada chipukizi katika tansinia ya bongo fleva anaefahamika kwa jina la Hadatha Mylose ambapo baadhi ya watu waliweza kumfahamu kupitia nyimbo yake ya “Legeza”.

Binti ambaye anakipaji kikubwa cha kutunga mashairi na kuimba ambavyo vinamfanya ajivunie, Hadatha ni msanii ambaye amatamamanio makubwa sana ya kuwa mwanamuziki mkubwa duniani akianza na bara la Africa

Safari yake ya kimuzikia ilianzia mkoa wa Ruvuma kupitia mashindano yanayofahamika kwa jina la “Smart Gean Challenge” ya mwaka 2020 mwezi wa nane, ambapo mashindano hayo yalimpa chachu ya kupambania kipaji chake mpka mwaka jana mwezi wa saba alipo amua kutoa ngoma yake ya kwanza ya chocho ambayo inafanya vizuri kupitia mitandao ya kijamii.

Lakini Pia Usiku wa tarehe 19 june, Kupitia Record Label inayofahamika mwa jila la “IBCD BRAND” ilifanya Lounching rasmi ya msanii huyo ambapo waliandaa hafla walioipa jina la “HADATHA IN JUNE”

Changamoto anazo kumbana nazo

Kupitia mwananchiacoop Hadatha alifunguka kuhusu changamoto anazo zipitia kutokana nayeye bado ni chipukizi na kueleza kuwa “changamoto ya kwanza ni soko ukizingatia mimi ni msanii mchanga, Lakini pia changamoto nyingine ni sehemu ya production ili niweze kutoa ngoma kali jamii watakayo ikubali, ukizingatia ndoto yangu kubwa ni kuwa msanii mkubwa ambaye natamani nifahamika ndani na nje ya nchi” Amesema Hadatha Mylose.

Eeeeeeeh! Kila mwanadamu kuna yale mambo anayo yapenda na asiyo yapenda mrembo huyuo alifunguka bwana na kueleza kuwa “kwanza Sipendi ugomvi, kugombana na mtu yoyote ikitokea kuna ugomvi kwangu huwa ni bora kukubali kushindwa kuliko kuanza kureact kuchochea ugomvi, na kuhusu kitu ninachokipenda bwana ni napenda sana kucheza michezo kama karata napenda kuogelea na kula pia, sasa hapa kwenye kula pia napenda kupika na najua haswa kupika” Amesema Hadatha.

Maisha ya mahusiano

Haya wale kaka zetu wanaomfukuzia mrembo huyo ameeleza kuhusu maisha yake ya mahusiano kwamba vijana mkae kwa kutulia binti hataki mbambamba hahaha make hapa kwanza ncheke bwana alifunguka mrembo huyo kuwa “Niko single sijaolewa na wala sitarajii kuolewa kwasasa nina focus kwenye muziki ili niweze kutoboa na mimi” amesema Hadatha Mylose 

Histoaria fupi ya Hadatha

Aidha mwanadada huyo alifunguka machache kuhusu historia yake ya elimu nk “Mim ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu ambapo mimi nikiwa dada mkubwa wa familia, Nimezaliwa Iringa na nimekulia Ruvuma , primary nimesoma mkoa wa Ruvuma wilaya ya Songea mjini katika shule ya Mjimwema Lakini secondary nimesoma mkoa wa Mbeya katika shule ya Nzondahaki hivyo level ya elimu yangu ni secondary” amesema mrembo Hadatha

We have accepted this beauty because she is a woman who lives by her dreams and loves what she does, she deserves to be in the mwanachiscoop magazine so we advise and encourage young women with dreams to get far not necessarily in music they can fight for their dreams and fulfill them as well.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post