GUESS WHAT! Your friends are your career network!

GUESS WHAT! Your friends are your career network!

Umewahi sikia msemo wa “YOUR NETWORK IS YOUR NETWORTH?’ Katika zama hizi za digital development, ni rahisi sana kufahamiana na watu wengi ambao, hata hivyo, wanaweza wasiwe marafiki wala kuwa na msaada kwako. Plus, its easy kufananisha your followers na your friends, so kuwa makini! Your way to career success ni kuwa na a career network.

Unaweza, kuwa na followers hata zaidi ya 10,000 kwenye mitandao ya kijamii, lakini usiwe na rafiki hata mmoja ambaye anaweza kukusaidia kufikia malengo yako.

Leo kupitia karia tunakufichuliwa siri ya kupata marafiki wa karibu watakaokuwezesha kufikia malengo.

Siri ambayo naifichua ni urafiki na malengo, mara nyingi marafiki zetu tulionao wamekua ni sehemu kubwa sana ya kutufanya either tufikie au tusifikie malengo tuliojiwekea.

Marafiki ambao watakufanya uweze kufikia malengo yako ya kufanya vizuri darasani, kupiga hatua kwenye biashara ni wale ambao wamekuwa wakikutia moyo pale unapoonekana kukata tamaa.

Pia ni wale watakaokushauri, kukurekebisha wakati unapokosea, kukufariji, kushirikiana na wewe nyakati za huzuni na furaha, kwa hiyo rafiki ana mchango mkubwa katika maisha yako.

Unapaswa kufahamu pia rafiki uliyenaye anayachukuliaje maisha, mafanikio na mambo yako mengine ambayo kwako ni muhimu, kwa kujua hivyo ni rahisi sana kumshirikisha mambo yako na yeye kukushirikisha ya kwake.

Pia hakikisha mara zote rafiki uliyenaye anakusaidia kufanikisha au kuboresha jambo furani la kimaendeleo ambalo unalo na wewe unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

Building a strong career network itakusaidia sana kupata opportunities mbalimbali hasa utakapo anza kazi. Ni marafiki watakaokutonya kuhusu nafasi za kazi, wapi kuna mishahara ya kuridhisha and the likes.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags