Gordon alimruhusu mkewe achepuke kutokana na umri wake

Gordon alimruhusu mkewe achepuke kutokana na umri wake

Aliyekuwa mume wa mtangazaji kutoka nchini Marekani Mia Thrnton, Gordon Thornton amefunguka na kueleza kuwa aliwahi kumruhusu aliyekuwa mkewe kuchepuka na mwanaume mwingine kwa sababu alijua kuna muda hatoweza kumtimizia haja zake kutokana na umri wake.

Kwa mujibu wa Page Six News inaeleza kuwa Gordon alimruhusu mkewe awe huru kuchepuka nje lakini asifanye kuwa matangazo liwe suala binafsi na asiwahusishe watoto wake na mahusiano yake na wanaume wengine.

Wanandoa hao wameachana September mwaka huu baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka 11 wakiwa wamebahatika kupata watoto 2, huku sababu ya kuachana kwa wawili hao ikiwa ni mwanaume huyo kufilisika.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags