Goodluck Ligogodor: Aeleza kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi chuoni

Goodluck Ligogodor: Aeleza kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi chuoni

Heyyyh! Vipi chuo kinapanda pande hizo au ndo tia maji tia maji, oky tuachane na hayo, kama kawaida yetu katika segmenti ya unicorner leo tumekusogezea  mada ambayo itakupa ufahamu haswa wale wanafunzi wanaopenda kuwa viongozi chuoni.

Uongozi chuoni kwa upande mwingine ni mzuri unakusaidia wewe ulieingia katika nafasi hiyo kujiweka karibu na mafanikio na kujichakarisha kwa pamoja, lakini siku zote katika mambo mazuri kuna mabaya pia ndo maana katika kila jambo kuna changamoto, faida na hasara.

Uongozi ni karama ambayo kila mtu huzaliwa nayo kwaajili ya kujiongoza lakini pia kuwaongoza wengine, karama hii ya uongozi hujidhihirisha katika makuzi ya kila mtu, kuna wale ambao huweza kujiongoza wenyewe tu na kuna wale wengine ambao wana uwezo wa kuwaongoza wengine pia.

Kwa hiyo ili mtu aweze kuwaongoza wengine inampasa kwanza aweze kujiongoza mwenyewe, katika makuzi na hatua mbalimbali za ukuaji mtu anazozipitia, karama hii ya uongozi hujionesha dhahiri pasipo kificho chochote.

Kuanzia ngazi ya chini kabisa ya shule ya awali, shule ya msingi, Sekondari hadi vyuoni ambapo siasa hushika hatamu ya kipimo cha mtu kufaa kuingia uongozini na kuongoza watu wengi waliomuamini na kumchagua kua kiongozi wao kwasababu ya sera zake.

Sasa leo hapa nakusogezea zile changamoto ambazo wanakumbana nazo viongozi wa chuo, ili kujua kuwa jambo hili ni serious kidogo nimekusogezea mwanafunzi wa chuo ambae pia ni kiongozi atatueleza kuhusiana na changamoto hizo wanazokumbana nazo.

Goodluck Ligogoderi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha afya na sayansi shirikishi muhimbili (MUIHASSO), akiwa anachukua kozi ya teknologia ya mionzi, ambae pia ni waziri mkuu katika serikali ya wanafunzi ya chuo hicho.

Uongozi wa wanafunzi vyuoni hua unafuatana kabisa na uongozi wa nchi yaani Serikali ya nchi, kwa maana huundwa na Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi, Baraza la Mawaziri, Spika wa Bunge anaewaongoza wabunge na Jaji Mkuu anaeongoza Mahakama ya Serikali ya wanafunzi.

Hivyo mfumo huu huunda Mihimili Mikuu mitatu ya Serikali yaani Serikali Kuu, Bunge na Mahakama.

Katika kila jambo hasa uongozi huwa na changamoto zake tofauti tofauti za kiutendaji, kihali na kimali halikadhalika ambazo husababisha mambo mengi ya kiserikali yasiende kadiri ya sera za viongozi husika na mahitaji ya wanafunzi kwa ujumla.

“Changamoto kubwa iliyopo ni changamoto ya kifedha ambapo baadhi ya vyuo hupata shida hiyo kwasababu ya mifumo ya kuendesha serikali ya wanafunzi kutokua rafiki na kupelekea viongozi kuchukua hatua ya kutumia fedha zao binafsi kwaajili ya kuendesha shughuli za kiserikali” amesema Goodluck

Aisha aliendelea kwa kueleza kuhusiana na changamoto ya kiuchumi ambayo hupelekea viongozi kutokupata posho ya kuwapa motisha ya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hivyo basi kupelekea hata yale mazuri yaliyokua ni matamanio yao kuyatekeleza kipindi cha uongozi wao kushindwa kutimilizika ipasavyo kwa namna moja au nyingine.

Uchaguzi wa vyuoni hua bora kwa kiasi kwasababu wanafunzi wanachagua kiongozi kadiri ya walivokua wanaishi nae na kushirikiana nae katika nyanja mbalimbali.

Hivyo kupelekea hata changamoto ya kuiba kura kwa mgombea aliyeshinda kuwa vigumu kwa maana uchaguzi wa Serikali ya wanafunzi husimamiwa na Tume huru ya Uchaguzi inayoundwa na wajumbe wanaotoka miongoni mwa wanafunzi.

Hahahahah! Kama nawaona wenzangu na mie wasiopenda sheria sheria maana hapo tumeskia kuhusiana mahakama, sijui bunge kuna watu ukizungumza hivi wanachanganyikiwa kabisa, lakini hii yote ni kwasababu ya kuelimishana na kueleweshana kuhusiana na swala sima la uongozi chuoni.

Alooooooh! I hope tumejifunza mengi kuhusiana na swala zima la uongozi chuoni, uzuri hatujazungumzia changamoto tuu tumezungumzia pia kuhusiana na kura katika uchaguzi, kwasababu kuna baadhi ya wanafunzi wanajua kuwa kula zinaibiwa lakini bwana Goodluck yeye ametuthibitishia hilo. Oky watu wangu wa nguvu tusiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop kwa ajili ya kujifunza Zaidi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags