Glory Fidelis: Biashara ya nywele imefungua milango lukuki ya mafanikio

Glory Fidelis: Biashara ya nywele imefungua milango lukuki ya mafanikio

Wewe unayeenda kuanza chuo au upo chuoni ujue kuna maisha baada ya chuo.

Ndio, lazima utambue hayo ili ukiwa chuoni hapo licha ya kuwa na uhakika wakupata hela baada ya miezi miwili kwa wale wenye Boom lakini hata kwa wale wasio nalo najua kuna namna mnapata pesa ya kujikimu so ni swali la kujiuliza baada ya kumaliza chuo utajiendeleza vipi.

Najua wengi wanasoma huku wakiwaza sana kuajiriwa mapema lakini nakuambia hakuna ajira ambayo ipo direct wazi inakusubiria wewe, swala la ajira ni bahati nasibu na hii asikudanye mtu kila ngazi now watu wapo mtaani.

Wanafunzi wengi hasa waliopo vyuoni wamekuwa wakiamini kuwa wakimaliza masomo yao na kugraduate ni rahisi sana kupata kazi au ajira.

Hata hivyo fikra hizo zimekuwa ni tofauti kwa Glory Fidelis mwanafunzi kutoka Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) aliyechukua Course ya Banking and Finance.

Glory amefunguka ndani ya MwananchiScoop na kuweka wazi jinsi biashara ya kusuka nywele aliyofanikiwa kuifanya kupitia fedha za boom ilivyofungua milango lukuki ya mafanikio.

Anasema kwake yeye alikataa kuamini kabisa katika masuala ya ajira bali amekuwa akiamini katika kupambana kwenye ufanyaji wa biashara na ndio maana milango ya mafanikio imefunguka kwake.

Glory anasema alifanikiwa kupata mkopo japo sio kwa asilimia 100 hivyo aliamua kugawa fedha hiyo kidogo kwa ajili ya matumizi binafsi na kuendeleza biashara yake hiyo kama kununua vifaa vya kazi ambavyo ni pasi ya nywele, hair curler, Gel, mafuta, rasta n.k

“Niliamua kuanza kufanya biashara chuo kwasababu ndio opportunity ambayo niliiona ningeweza kukuza kipaji changu na kufanya nikue zaidi kibiashara ingali bado mdogo,” anasema

Anasema kupitia biashara yake hiyo alifanikiwa kuwa sponsor wa mashindano ya Bongo Star Search mwaka 2020 akiwa bado mwanafunzi.

“Kwa kufanya hivi brand yangu ilikua zaidi...Pia nilifanikiwa kusponsor Bingwa show 2021....Nimefanikiwa pia mpaka sasa kufanya kazi na kampuni ya urembo iitwayo Atsoko.... mbali na kupata kazi ndani ya mwaka 2021 nilifanikiwa kutengeneza nywele bibi harusi (3) kazi ambayo sikuamini kama ningeweza kuifanya,” alisema.

Kitu kingine anachopenda kufanya

Hata hivyo anasema moja ya jambo ambalo analipenda kulifanya ni make up eapecially (special effect).

“Hii ni cinema make up ambayo hufanywa katika filamu mbalimbali. Nilijifunza tu kama utani lakini mwezi wa 11, 2021 ni msimu wa halloween nilifanikiwa kupata gigs za kutengeneza watu design mbali mbali kwa ajili ya maonyesho,” ALISEMA

Alisema kupitia kujifunza kwake make up alifanikiwa kusponsor filamu ya "Moto" iliyofanywa na Kampuni ya Tai plus mwaka 2021.

Changamoto

Anasema changamoto katika kazi yake hiyo ni wateja kutokuweza kufikia viwango vya bei ambazo anakuwa akizipanga kwa sababu wateja wake wakubwa ni wanafunzi.

“Wanashindwa kufikia bei kwa sababu, circle yangu kubwa ilikua wanafunzi ilinipasa kutengeneza bei zinazoendana na mazingira... mfano utakuta hairstyle ya sh. 50,000 kwa maisha ya chuo ni ngumu kupata mteja inabidi uweke 25,000 mpaka 30,000,” alisema.

Ushauri kwa vijana

Anasema anawashauri vijana wajitume zaidi wanapokua vyuoni kwani opportunity nyingi zinapatikana wakiwa bado wanasoma na kuongeza kuwa wajifunze kupangilia ratiba zao vizuri maana kuna maisha baada ya chuo.

“Pia wasiwe tegemezi watumie vipaji walivyonavyo kuanza na ulichonacho na hapo ulipo ndio jambo la msingi usisubiri baadae,” alisema.

Pia alisema kwa miaka ya baadae anatamani kuwa mama bora kwa watoto wake kwani bila wazazi wake kuwa bora kwake asingekua kama alivyo leo.

“Imekua inspiration kutoka kwa wazazi wangu jinsi walivyonilea katika maadili mazuri, kiukweli natamani san akuwa kama wao ili nami niweze kuwa na watoto bora wenye kujituma kila wakati, alisema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post