Gladness kuinua wanawake wenye vipaji

Gladness kuinua wanawake wenye vipaji

Mchekeshaji na muigizaji kutoka nchini Gladness Kifaluka maarufu kama Pili Wa Kitimtimu ameweka wazi kutaka kuinua wanawake wenye vipaji vya uchekeshaji.

Gladness ameyasema hayo kwenye mkutano wake na vyombo vya habari ambapo ametangaza kuja na ‘Female Stand Up Comedian Search’ sehemu ambayo wanawake wataweza kuonesha vipaji vyao.

Huku lengo na madhumuni ya kufanya hivyo ni kuwashika mkono wanawake ambao wanavipaji lakini hawajapata watu wa kuwasimamia.

Hata hivyo kupitia mkutano huo pia ameweka wazi Majaji ambao watasimamia mtanange huo akiwemo mtangazaji na mfanyabiashara Zamaradi Mketema, Mpoki pamoja na Evans Bukuku.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags