Gigy Money aitamani ndoa

Gigy Money aitamani ndoa

Moja ya story inayobamba mitandaoni huyo ni ya msanii Gigy Money ambaye ameshea ujumbe wa kutamani kuingia kwenye ndoa baada ya kunogewa kwenye penzi jipya na mwanaume wake mpya.

Gigy Money ameandika ujumbe huo kupitia Instagram yake kwa kupost video clip akiwa na mwanaume wake huyo anayefahamika kwa jina la Crey.

"Mapenzi ni ujinga ndio maana sipendagi kabisa kujigusisha haya tayari nimeshapenda tena, yaani nikipenda huwa boya na mjinga kishenzi hapa najiona nina miaka miwili etiii khaaaa sitoboi" ameandika Gigy na kuongeza

"Tena marafiki zangu nisameheni, tulikubaliana hatumpost mpenzi 'this time but' nimeshashindwa kuficha hisia mie, si mnanijuaa napenda vibaya nisameheni tu, sema nakukubali sana mwanangu Crey"

"Tatizo sipo romantic ndio mana naibiwagwa ila kichaaa pia nimejaribu kuwa sweet uwe wa mwisho katika maisha yangu yani unioe, sio saiv miaka hata 27 huko".






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags