Gigy money aingilia kati ugomvi wa Shilole, Alikiba

Gigy money aingilia kati ugomvi wa Shilole, Alikiba

Kila mmoja anajua kinachoendelea mitandaoni kati ya Alikiba na Shilole baada ya Kiba kusema hakumualika Shilole kwenye uzinduzi wa Album yake.

Shilole hakukaa kimya alikuja juu na kuhoji kwanini Alikiba anasema hivyo haliyakuwa alimpost kwenye page yake ya Instagram.

Mmoja wa mastaa wa Bongo Fleva Gigy Money hajakaa kimya amekuja mitandaoni na kutoa maoni yake kuhusu hilo.

Gigy amesema Alikiba hakupaswa kuongea hadharani juu ya suala hilo na kusisitiza kuwa yeye yupo upande wa Shilole na ataendelea kumla sapoti  mwanadada huyo.

 







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags