George alikataa kuwepo kwenye video ya Nicki

George alikataa kuwepo kwenye video ya Nicki

Nyota wa NBA kutoka nchini Marekani Paul George ameweka wazi kuwa alishawahi kukataa ombi la ‘rapa’ Nicki Minaj kuwepo katika moja ya ngoma zake.

Paul alifunguka suala hilo kupitia mahojiano yake na ‘Padcast P’ ambapo alieleza kuwa ilikuwa ni kama miaka miwili au mmoja uliopita Nicki alimfuata ili aweze kuwepo kwenye moja ya video yake ambapo alidai kuwa alimkatalia, kutokana na ratiba zake kubana.

Aidha aliongezea kwa kusema kuwa endapo angekubali kufanya video na Nick basi siku hiyo angekwenda na mkewe Daniela.

Paul George nyota wa mpira wa kikapu anayekipiga katika ‘timu’ ya ‘Los Angeles Clippers’ kwasasa amefikisha point 22 kwenye msimu huu wa NBA.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags