Gary Neville amuwakia Rais wa Fifa

Gary Neville amuwakia Rais wa Fifa

NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville ameibuka na kumtaka Rais wa FIFA Gian Infantino kujisafisha kutokana na kauli tata alizozitoa siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Neville amesema Infantino kama Rais wa FIFA na anayewakilisha taasisi kubwa ya kimichezo duniani hakupaswa kutumia lugha na maneno yale aliyotumia kwani hayajengi na hasa yanasababisha mpasuko na mtengano katika jamii ya mataifa mbalimbali ambayo mchezo wa mpira wa miguu unayaweka pamoja.

“Nimekuwa maeneo mbalimbali Duniani nikiwa na klabu ya Manchester United Mashariki ya kati, Mashariki ya mbali, Asia, Afrika na Australia lakini Hapana shaka mpira wa miguu unatakiwa tuupeleke kila eneo duniani kote.

Lakini ni mtu wa ajabu sana kwenye soka letu (Infantino) baadhi ya mambo aliyoyasema hayakuwa na msingi na hayakupaswa kusemwa kutoka kwa mtu wa hadhi yake, anapaswa kuwa kama mtu wa serikalini, anapaswa kuwaleta watu pamoja yeye ni muwakilishi wa mpira wa miguu duniani.” Alinukuliwa Gary Neville na Kituo cha Televisheni cha beIN Sport.

Mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia yalianza rasmi jana ambapo mwenyeji Qatar alicheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Ecuador na matokeo kumalizika kwa mwenyeji kukubali kichapo cha mabao 2-0, mabao yote yalifungwa na mshambuliaji tegemeo wan chi hiyo Enner Valencia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags