Gara B, Dokta Cheni wanavyobamba na nyimbo za wasanii wakongwe

Gara B, Dokta Cheni wanavyobamba na nyimbo za wasanii wakongwe

Ukisikia cha kale dhahabu ndiyo hiki, kwa sasa kwenye sherehe kama vile harusi, 'Send Off' na 'Kitchen Party' siyo ajabu kusikia ngoma za zamani zikipigwa na wageni waalikwa wakiruka nazo.

Nyimbo kama ‘KimyaKimya’, ‘she got a gwan’ (Mangwea), ‘Mkono moja weka juu’ (Chege Chigunda), ‘Nikusaidiaje’ (Profesa Jay), ‘Dar Stand Up’ (Chid Benzi), ‘Fagio la Chuma’ na nyinginezo ni ngoma zinazotumika mara kwa mara.

Kutokana utumiwaji wa ngoma hizo za zamani Dokta Cheni ambaye amekuwa MC kwenye sherehe kadhaa, amesema kupigwa nyimbo za zamani kwenye ni upepo wa kujaribisha kitu na kuona kama watu watakipokea.

“Kupigwa nyimbo za zamani kwenye event ni upepo tu ambao watu wanajaribu na kuona kama kitaweza kupokelewa na wananchi na watu wanatakiwa wajue siyo redio wala televisheni zinaweza kurudisha nyimbo za wasanii wa zamani hata sisi ma-Mc tuna nafasi hiyo kubwa sana.

"Nilishawahi kukutana na mwanamuziki mmoja nimemsahau jina nikamwambia ukikutana na ma-Mc wakapiga ngoma zenu ujue zitakubalika sana kwa sababu ma-Mac tuna-support vitu hasa vinavyohusu muziki,” amesema.

Pia ameelezea kupiga ngoma za zamani ni kuongeza thamani kwa wasanii wakongwe ambao wengine tayari wameshapotea kwenye muziki.

“ Sisi tunawaongezea thamani wasanii wakongwe kwa mfano sasa hivi tunapiga ngoma za Q Chief, Juma Nature, Profesa Jay, yaani zipo nyingi ambazo hata kwenye radio sasa hivi walikuwa hawapigi hadi nyimbo za Kina Marijani Rajabu,” amesema Cheni.

Hata hivyo, ameeleza kuwa kupitia wao wasanii wakongwe wanaweza kupata show mbalimbali kama wa kizazi kipya.

“Kupitia sisi kupiga ngoma zao wasanii wakongwe sasa hivi wanaweza wakapata show nyingi kama wasanii wa sasa hivi, hii kauli yangu ishike kwa makini kwa sababu tumekuwa kama tunawaamsha watu kufuatilia ngoma za zamani,” amesema.

Mbali na hayo, Cheni amesema mwanzoni wakati wanaanza kupiga ngoma za zamani kwenye siyo watu wote walikuwa na muitikio ila kwa sasa asilimia kubwa ya rika zote wameonekana kuzielewa."

Kwa upande wake Mc Gara B, amesema katika sherehe kuna rika tofauti hivyo lengo la kupiga ngoma za zamani ni kuwapa ladha kila aina ya hadhira kwenye matukio.

“Unajua kwenye sherehe kunakuwa kuna watu wa rika zote so lengo la kurudisha ngoma za zamani ni katika ku-cover kila aina ya audience katika ukumbi ila wakati mwingine tuna angalia aina ya audience ni watu wa aina gani maana kuna watu walikuwa wana 'enjoy' nyimbo za kina Dully Sykes na Professor Jay na Chemba Squad unawawekea.

"Pia kuna watu ambao wanapenda nyimbo za sasa za Amapiano tunawawekea wanacheza macho juu lengo ni katika kuwafurahisha watu wote,” anasema Gara B.

Aidha Gara B, ameeleza kuwa kupiga muziki wa zamani ukumbini kwake inamuongezea thamani kwa sababu watu wanapenda.

“Inanipa thamani sana kwa sababu mteja wangu akishafurahi tayari pale najua simu zitaita akiwa na jambo lake tena kwa sababu atakuwa tayari kunilipa kiasi chochote ninachokitaka na wakati mwingine hataki hata kupunguziwa ili mradi tu ampate Gara B kutokana na kazi yangu nzuri,” amesema.

Mbali na hayo ameeleza watu wamekuwa wakizipenda nyimbo hizo kwenye event kwa sababu kuna baadhi ya vitu wanavikosa katika nyimbo za sasa.

“Kitu ambacho watu wanakosa kwa sasa ukilinganisha na nyimbo za zamani, ukiangalia nyimbo za sasa hivi unaweza kukuta ni fupi halafu maneno yanajirudia hasa katika nyimbo za Amapiano lakini nyimbo za kipindi hicho unakuta kama ni stori kutokana na mashairi yake yanakuwa yanajitosheleza.

Sababu ya wanamuziki wa sasa hivi kurudia maneno vijana wsasa hivi wanafanya muziki wa biashara so wanaangalia maokoto, apate shows na aweze kuuza kwenye Digital platform na soko ndiyo ilinavyo taka hivyo” amesema Gara B.

Gara B ameeleza kuwa hakuna Mc aliyeanzisha kuweka playlist za nyimbo za zamani katika sherehe ambapo amedai kuwa ilikuwepo muda sana anasimulia.

“Huu mtindo ulikuwepo tokea muda ni kwa sababu sisi wengine tumekuja ku-post hivi karibuni lakini ilikuwepo hivyo kama Mc inabidi uangalie watu wako wanataka nini.”

Mc Big Chris anaye ameongezea kwa kusema mtindo wa kupiga nyimbo za zamani hauja anza kwa ma Mc peke yake bali ilikuwepo hata kwenye kumbi za starehe na lengo ni kuwakumbusha watu enzi zao.

“Huu mtindo sio kwa ma Mc peke yake hata kwenye kumbi za starehe pia wamekuwa wakifanya ambapo ‘MaDj’ wana pika nyimbo hizo kwa kuwa kumbusha watu enzi zao kwa sababu ukiangalia nyimbo za sasa zinazopigwa ni za vijana tu ila kuna kizazi cha katikati kina kuwa kimesahaulika,” anasema.

Hivyo ameelezea kuwa nyimbo za zamani zilikuwa zina maadili ambazo unaweza ukasikiliza ukiwa sehemu yeyote na kumkumbusha mtu historia ya nyuma.

“Kwanza nyimbo za zamani zilikuwa na meseji ambazo zimesimama na unaweza ukasikiliza na kuimba mbele ya baba au mama bila shida yeyote na ndiyo maana sasa hivi zikipigwa lazima watu wasimame wa-vibe mbele ya mtu yeyote,” anasimulia.

Mc Big Chris alienda mbali zaidi akidai kuwa yeye huwa anapanga muda wakupiga nyimbo za zamani katika sherehe ambapo anaweza kuwainua watu kwenye viti.

“Kingine ni ubunifu tu ambao mtu binasfi unaweza ukafanya kwa kutenga muda fulani ambao unahisi nikipiga nyimbo hizi nita wanyanyua wazee na wanaopenda kusikilizaq nyimbo za zamani kama zilipendwa na zile Bongo fleva za zamani” anasema

Hata hivyo, ameeleza namana inavyompa thamani ambapo amesema kuna wateja wengine huwa wanamfuta kwa sababu yeye Playlist yake," anasimulia.

“ Mimi huwa inanipa value kwa sababu mteja ananifuata na kutaka kazi yake kwa kuwa ameona kitu na anakwambia kabisa kuna nyimbo fulani hataki kuzi sikia au nyimbo zenye matusi hataki na nyimbo zenye mafumbo kwa hiyo nimbo za zamani nazo zina tu value unakuta zime nyooka na hazina hivyo vitu,” amesema.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post