Gadiel ajutia uamuzi wa kuondoka Yanga

Gadiel ajutia uamuzi wa kuondoka Yanga

Kuna msemo wa kukosea ni wakati wa kwenda sio kurudi. Hii ni kauli inayomlenga Gadiel Michael ambaye amezitumikia ‘timu’ tatu kubwa za ‘Ligi’ Kuu Bara.

#Gadiel alianzia #AzamFC iliyomlea na kumpa mwanga kuonekana zaidi kwa ‘timu’ za Kariakoo akianza kukipiga #Yanga misimu miwili na baadaye #Simba.

Mwanaspoti limefanya mahojiano na staa huyo ambaye ana uhakika wa namba #SingidaFountainGate na kafunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujutia uamuzi wa kutoka Jangwani na kutua #Simba.

“Katika maisha yangu ya ‘soka’ kitu ambacho sitakaa nikakisahau ni kuondoka #Yanga baada ya kuitumikia kwa miaka miwili na kutua #Simba nikiamini nitatimiza malengo yangu,” anasema.

“Kuondoka #Yanga halafu nilipokwenda sikufikia malengo niliyotarajia ni moja ya tukio ambao sitakaa nikalisahau kwani lilinipotezea mwelekeo. Nashukuru nimerudi kwenye mstari na naanza kujitafuta upya.”

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags