Furahi yaendelea kumpa kiburi Makabila

Furahi yaendelea kumpa kiburi Makabila

Mwanamuziki wa Singeli nchini Dulla Makabila, ameendelea kujipakulia minyama kutokana na wimbo wake uitwao 'Furahi' kukamatia namba moja kwenye mtandao wa YouTube kwa zaidi ya siku tatu mfululizo.

Wimbo huo uliweza kuingia namba moja kwenye mtandao wa YouTube kabla ya saa 20 jambo ambalo linamfanya Dulla aendelee kuvimba, na sasa anajiita mfalme wa singeli.

Kupitia mtandao wa Instagram msanii huyu ameshusha ujumbe ukieleza kuwa yeye ndiye mfalme wa muziki huo, kwa sababu tangu dunia ianze wimbo wake ndiyo wa kwanza kwenye upande wa singeli kuingia trending namba moja kabla ya saa 20.

Hata hivyo Dulla amewataka wasanii wengine kujifunza kutoka kwake kwani anaamini kuwa maendeleo hayana chama. Hadi sasa 'Furahi' bado upo namba moja YouTube na kufikisha watazamaji 624k huku ukiwa na siku sita tu tangu utoke.

Ikumbukwe kuwa wimbo huo ndiyo ulipelekea juzi Januari 24, Makabila kutakiwa 'kuripoti' kituo cha polisi cha Oysterbay kwa ajili ya mahojiano, baada ya kudaiwa mistari ya wimbo huo inamlenga aliyekuwa msemaji wa Yanga Haji Manara na mkewe Zaiylissa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags