Fred Omondi afariki dunia

Fred Omondi afariki dunia

Fred Omondi ambaye ni mdogo wa mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Eric Omondi amefariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari.

Kwa mujibu wa tovuti ya Pulse, Fred amefariki dunia asubuhi ya leo Juni 15, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mama Lucy iliyopo jijini Nairobi.

Fred ambaye pia ni mchekeshaji alipata umarufu alipokuwa akifanya kazi katika kipindi cha ‘Churchill Show.’
Kupitia mahojiano enzi za uhai wake alisema kaka yake Eric ndio alimvutia yeye kuingia kwenye uchekeshaji.

Fred aligongwa na gari jana jioni Juni 14 2024, akiwa kwenye bodaboda wakati alipokuwa anaelekea nyumbani kutoka kwenye majukumu yake.

Ikumbukwe kuwa mchekeshaji huyo baada ya kuacha kufanya Starnd up Comedy kwenye ‘Churchill Show’ miaka michache iliyopita alianza kufanya kazi kama MC.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags