Frank Gervas  Kiu yangu kubwa kucheza soka la kulipwa

Frank Gervas Kiu yangu kubwa kucheza soka la kulipwa

Harakati za maisha, kupambana na kuhakikisha unayafikia malengo uliyojiwekea sio jambo la kispotispoti mtu wangu, tafakari jitoe uwezavyo bila kujali maslahi ya haraka kwani katika safari ya mafanikio kuna hitaji uvumilivu mkubwa.

Hivyo ndivyo ninavyomaliza wiki hii ikiwa tunaufukuzia mwezi wa 9 bwana, ukiwa unayoyoma kimtindo. Ebwana leo ni furahiii day kama kawa kama dawa, ile siku ya makala za burudani pamoja na michezo lakini wiki hii bwana namsogeza kwako kijana mahiri kabisa, Frank Gervas.

Huyu ni kijana kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT akiwa anachukua Bachelor degree in Information Technology, mwaka wa tatu chuoni.

Licha ya elimu hiyo ambayo anapambania kutafuta kwa sasa Frank ni kijana mwenye kipaji na uwezo wa kucheza mpira wa miguu.

Akizungumza na jarida la Mwananchi Scoop, Frank ameeleza sababu za vijana wengi hasa wa kiume kupenda na kushabikia mpira wa miguu akidai kuwa ndiyo mchezo maarufu zaidi duniani na una mashabiki wengi hivyo huvutia watu.

Vilevile alisema kuwa mchezo huo unaushabiki ndani yake ndiyomaana watu wengi huwa wanatimu zao ambazo ziwapa motisha wakuufatilia zaidi mchezo huo.

Samabamba na Frank ni kijana nayejali sana suala zima Muda kwani ndiyo kiapaumbele chake, akiamini Muda ndiyo unaozungumza kila kitu katika harakati za kimaisha.

Aidha alisema kuwa football ndiyo mchezo ambao yeye anakubali zaidi licha ya kuwepo michezo mingine lakini huo umekua kivutio kikubwa kwake.

Vilevile alielezea siri kubwa ya kuuelewa mchezo huu alibainisha kuwa kadri unavyojifunza ndivyo unavyoweza kufanikiwa zaidi, kwani kupitia mchezo huo ameweza kuongeza familia mpya.

Nikukumbushe tu Frank ni Mwanafunzi huyu hapa anazungumzia changamoto mbalimbali anazokutana nazo katika safari yake ya elimu pamoja na kipaji alichonacho.

“Binafsi yangu mimi changamoto kubwa sana kwangu ni shule kwani shule inachukua nafasi kubwa sana kuliko kitu chochote japo napambana ili kuhakikisha sipotezi kote”alisema.

Sambamba na hayo Frank anamalengo aliyojiwekea kupitia kipaji alichonacho hasa anapigania hapo baadaye aweze kucheza soka la kulipwa.

“Mimi malengo yangu ni kuja kucheza soka la kulipwa na hii naamini ni ndoto ya kila kijana ambaye anajihusisha na mpira wa miguu wote tunapambania kwenye hilo”alisema.

Hata hivyo alizungumzia namna mchezo huo ulivyoweza kumpa manufaa tangu alipoanza kucheza hadi hapa alipofikia sasa.

“Mpira umeninufaisha kwani mimi naamini katika watu sana mafanikio kila kitu kipo kwa watu mpira umenipatia familia kubwa sana umenipatia watu sahihi kwa moyo wangu mimi naona sawa kuwanao”alisema.

Je umewahi kúpata medal yoyote?

“Yah  ofcourse nimewahi kupata medali na namshukuru Mungu nimeshapata medali kama tatu hivi moja wapo ambayo ni kubwa ni ile niliyoipata baada ya kuwa mfungaji bora wa mashindano ya Shingvuka haya ni mashindano ya vyuo”alisema.

Hata hivyo frank anaamini zaidi katika mafanikio malengo yake makubwa baada ya kufikia ndoto zake anatamani sana kuja kuwashika mkono vijana wengine hasa wale wenye vipaji.

Je wewe unapenda Nini ?

“kiukweli mimi napenda sana watu wakipendana, watu wakipeana michongo wakisuportiana kiukweli napenda upendo that’s all”alisema.

Turudi nyuma na tuende mbele sasa kila mmoja katika maisha haya anajambo lake ambalo linampatia amani katika moyo wake lakini kwa kijana huyu unafahamu ni kitu gani kinampa amani zaidi katika maisha yake?

“Kitu ambacho mimi kinanipa amani ni upendo wa Mungu, kiukweli upendo wake unanipa amani mnoo kwenye maisha yangu hakuna jengine”alisema.

Ebwanaaa eeeh!! Hayo ndiyo maisha halisi ya kijana Frank Gervas kutoka chuo cha usafirishaji akiamini zaidi katika soka la kulipwa hapo baadaye ikiwa ndiyo kiu yake kubwaa.

Enheeee!!! Tuambie kijana unayesoma makala haya na kama mdau wa michezo wewe kiu yako uiko wapi zaidi katika mpira wa miguu? Have a nice weekiend!!!!!!!!!!.






Comments 4


  • Awesome Image
    Frank gervas

    Thanks for interview...hakika it was marvelous 🙏

  • Awesome Image
    Frank gervas

    Thanks for interview...hakika it was marvelous 🙏

  • Awesome Image
    amad

    alikuwa mfungaji bora wa shimivuta ya mwaka gani na ilifanyika...???

  • Awesome Image
    amad

    alikuwa mfungaji bora wa shimivuta ya mwaka gani na ilifanyika...???

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags