Filamu ya Travis yageuka gumzo

Filamu ya Travis yageuka gumzo

Baada ya mwanamuziki kutoka nchini Marekani Travis Scoot kufanya vizuri kwenye muziki wa hip-hop, kwa kutoa ngoma kali kama vile ‘My Eyes’, ‘Butterfly Effect’na ‘Thank God’, sasa amehamia kwenye ulimwengu wa filamu.

Licha ya filamu nyingi zenye ubora wa video kuongoza kununuliwa kwenye vituo mbalimbali vya kuonesha kazi hizo, lakini kwa mkali huyo wa hip-hop imekuwa tofauti kwani ameachia filamu mpya iitwayo ‘Aggro Dr1ft’ ambayo video yake haioneshi wahusika kwa ubora .

Trela la filamu hiyo ambayo imeachiwa siku chache zilizopita imezua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii baada ya video kuwa na rangi mbalimbali (infrared) zinazozuia wahusika kuonekana vizuri.

Filamu hiyo imeongozwa na Harmony Korine huku starring akiwa Jordi Mollà na Travis Scott mwenyewe.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags