Filamu ya Tiwa kuanza kuonekana mei 10

Filamu ya Tiwa kuanza kuonekana mei 10

Mkali wa afrobeat kutoka nchini Nigeria Tiwa Savage ametangaza kuwa filamu yake ya ‘Water and Garri’ itaachiwa rasmi Mei 10 mwaka huu, itaruka kwa mara ya kwanza kupitia Prime Video.

Kwa mujibu wa muongozaji wa filamu hiyo Meji Alabi, ameeleza kuwa ‘Water and Garri’ ni filamu ya kwanza kutoka nchini Nigeria inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki kutoka katika nchini zaidi ya 240.

‘Water and Garri’ ni filamu ambayo inasimulia maisha halisi ya mwanadada Aisha (Tiwa) ambaye ni mbunifu wa mavazi aliyetumia miaka 10 nchini Marekani ambapo inambidi arudi nyumbani kwao kwa ajili ya msiba wa mmoja wa familia yake lakini anakuta maisha ya nyumbani kwao yamebadilika vurugu zimeongezeka.

Hata hivyo Water & Garri ni jina la EP ya nyimbo tano za Savage iliyotoka mwaka 2021, huku mastaa ambao wataonekana katika filamu hiyo ni Jemima Osunde na Mike Afolayan.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags