Filamu Ya Squid Game Season 2 Yaweka Rekodi

Filamu Ya Squid Game Season 2 Yaweka Rekodi

Filamu maarufu inayokimbiza zaidi Duniani kote ya ‘Squid Game’ msimu wa pili imeripotiwa kuweka rekodi kwa kushika namba moja kwenye nchi zaidi ya 93.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes imeeleza kuwa ingawa hakuna idadi kamili ya ni watu wangapi wameshaitazama filamu hiyo lakini imeripotiwa kuweka rekodi ambayo haijawahi kutokea dunaini kote kwa kushika namba moja katika nchi 93 huku nchi ambazo ziko juu zaidi ni Marekani, Honduras, Kenya, Oman, Thailand na nyingine.



Aidha licha ya msimu wa kwanza wa Squid Game kuweka rekodi ya kupata watazamaji zaidi ya bilioni 2.2 ndani ya lisaa limoja lakini pia inaelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa msimuu huu wa pili kupata watazamaji wengi zaidi.

Utakumbuka msimu wa kwanza wa Squid Game ulishinda tuzo sita za Primetime Emmy, ikiwemo tuzo ya kihistoria kwa mkurugenzi Hwang Dong-hyuk, ambaye alishinda tuzo ya Outstanding Directing kwenye kipengele cha Drama Series.

Squid Game msimu wa pili iliachiwa rasmi Desemba 26, 2024 huku ikichezwa na mastaa mbalimbali wakiwemo Lee Jung-jae, Lee Byung-hun, Wi Ha-jun, na Gong Yoo.

Huku kukiwa na washiriki wapya kama Yim Si-wan, Kang Ha-neul, Park Gyu-young, Lee Jin-uk, Park Sung-hoon, Yang Dong-geun, Kang Ae-sim, Lee David, Choi Seung-hyun, Roh Jae-won, Jo Yu-ri, na Won Ji-an.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags