FDA yatoa kibali kuanzisha majaribio ya kupandikiza ubongo bandia

FDA yatoa kibali kuanzisha majaribio ya kupandikiza ubongo bandia

Kampuni ya Neuralink inayomilikiwa na bilionea Elon Musk imepata kibali cha mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) kufanya jaribio la kwanza kwa binadamu baada ya kufanya upandikizaji huo kwa wanyama.

Kwa mujibu wa taarifa za Neuralink, watu watakao pandikizwa kifaa hicho au wagonjwa wataweza kutumia ubongo bandia kwa njia ya programu itakayo unganishwa na Bluetooth na vifaa vingine vitakavyo ambatishwa baada ya upasuaji.

Teknolojia hiyo inayolenga kurejesha utendaji sahihi wa mwili kwa wenye matatizo ya mfumo wa neva ikiwemo kupooza baada ya ubongo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Pia inatarajiwa kuongeza uwezo wa ubongo kufikiri zaidi ya kiwango cha kawaida.

Vipi mdau uko tayari kuongezewa uwezo wa ubongo wako ili ufanye kazi zaidi ya sasa? tupia maoni yako mwanetu tuone mtazamo wako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags